LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 4, 2021

KANISA HALISI LAWAALIKA MACHINGA KATIKA IBADA MAALUM YA KUWABARIKI, ITAKAYOFANYIKA JUMAPILI HII, TEGETA JIJINI DAR ES SALAAM

Tegeta, Dar es Salaam
Baba Halisi wa Kanisa Halisi la Mungu Baba amewakaribisha Wafanya Biashara ndogondogo 'Machinga', katika Ibada Maalum ya kuwabariki Wafanyabiashara hao, ambayo itafanyika Jumapili hii, Novemba 7, 2021 (Lango la Moyo Mmoja, 19 Eluli 9), Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta  jijini Dar es Salaam.

"Wote Mnakaribishwa bila kujali Dini au Dhehebu maana Chanzo Halisi amekuja kuwabariki wote ( Efeso 4:6) amesema Baba Halisi katika Tangazo la mwaliko  wa Machinga kuwaalika wafike kwa wingi kwenye Ibada hiyo.

Ibada hiyo ya Kuwabariki machinga, itakuwa ya nne ya kijamii kufanywa na Kanisa hilo, ikiwa imetanguliwa na Ibada ya Kuwabariki Waandishi wa Habari, Ibada ya 'Kufuta ajali' kwa waendesha bodaboda na Ibada ya kuwabariki Mama na Baba Lishe kwa ajili ya kuleta 'jiko jipya', iliyofanyika Jumapili iliyopita.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages