LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 17, 2021

FAO YAWAPIGA MSASA WANAHABARI ATHARI ZA USUGU WA VIMELEA VYA MAGONJWA DHIDI YA DAWA (AMR)+video




Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Waziri Mkuu Menejimenti ya Maafa, Charles Msangi akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari kuhusu athari za usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa. 

Semina hiyo imefanyika leo Novemba 17, 2021 jijini Dodoma, ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya Wiki ya kuielimisha jamii kuhusu athari za usugu na jinsi ya kuepukana nao yanayoanza kuadhimishwa Novemba 18 hadi 24 nchini na duniani kote. 



Dkt. Andrew Kayuni kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, akifafanua jambo wakati wa warsha hiyzo/

Mgeni rasmi Charles Msangi akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari na baadhi ya maafisa kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo FAO mara baada ya kufungua rasmi warsha hiyo.
Mratibu wa Taasisi ya RBA - Initiative, Baritazar Stanley  akitoa mada kuhusu umuhimu wa kutoa elimu kwa jamii kuhusu athari za Usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya  dawa.
Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa makini mada zikiendelea kutolewa na wataalamu.

Mratibu wa Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa (AMR), wa Shirika la Kilimo Duniani (FAO), Dkt. Eribariki Mwakapeje akielezea maandalizi ya maadhimisho ya Wiki ya Kuelimisha Jamii kuhusu AMR.

Ofisa Mawasiliano wa FAO, Alice Maro akifafanua jambo wakati wa warsha hiyo.
Mratibu wa Sekta ya Mifugo Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Dkt Bertha Dugange (Phd), akichangia mada wakati wa warsha hiyo.


 Mfamasia Suma Jairo kutoka Wizara ya Afya, akifunga warsha hiyo ya waandishi.


PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii hapa chini, wataalamu kutoka sekta mbalimbali wakiwasilisha mada kuhusu Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa (AMR) katika warsha hiyo ya wanahabari....

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages