Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo amesema ni wakati sahihi kuwa na Sheria itakayowataka Vijana kuwatunza Wazee wao kama wao walivyotunzwa walivyokuwa watoto chini ya sheria ya haki za mtoto.
“Niseme hili jambo ni lazima tukalipitie na tukaliwekee sheria”
Chongolo ameyasema hayo alipokutana na Wazee wa Wilaya ya Chato ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua, kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Katika ziara hiyo katika mkoa wa Geita, Katibu Mkuu ameongozana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambapo kila mjumbe amepangiwa wilaya ya kutembelea.
Akiwa Wilayani Chato Katibu Mkuu na Ujumbe wake walipata nafasi ya kuzuru Kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli na baadae alifanya mikutano katika mashina matatu ambayo ni shina namba 30 Mwabasabi Kata ya Muungano, Shina namba 1 Mrumba Kata ya Bwina na Shina namba 13 Mkuyuni Kata ya Chato.
Aidha katika ziara hiyo Mbunge wa Jimbo la Chato Dkt. Merdad Kalemani ametoa pongezi na shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Mkuungano wa Tanzania kwa kuwapa zaidi ya bilioni 16 kwa ajili ya shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa madarasa mapya zaidi ya 100, barabara, vituo kwa afya na maboresho ya katika hospitali ya Kanda.
Hongera sana kwa kazi nzuri Katibu Mkuu na team nzima ya sekretarieti, CHAMA ni wanachama Kongole kwenu!!!
ReplyDelete