HABARI MPYA

Your Ad Spot

Saturday, October 23, 2021

WAZIRI WA ULINZI DKT TAX AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUPANDISHA BENDERA YA UN DODOMA+video

Wayiri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga, Dkt Stergomena Tax akishuhudia Bendera ya Umoja wa Mataifa (UN) ikipandishwa  wakati wa maadhimisho ya miaka 76 ya umoja huo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma leo Oktoba 23, 2021.

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini,,Zlatan Milisic akiwatambulisha maafisa UN kwa Waziri Dkt Tax.
Waziri Dkt Tax  akiwa amesimama kwa heshima wakati wimbo wa Taifa ukipigwa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kupandisha Bendera ya  UN .
Waziri Dkt Tax akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa maalumu kwa ajili ya maadhimisho hayo.


Baadhi ya viongozi wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa. 

Sehemu ya wananchi wakishuhudia maadhimisho hayo.
Gwaride la kikosi cha Jeshi la Wananchi likiondoka baada  shughuli ya kupandisha bendera ya UN kumalizika.

 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kuona kupitia clip hii ya video hapa chini Bendera ya Taifa ikipandishwa...
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

Tafadhali andika maoni yako kuhusu habari hiyo uliyosoma. Andika hapo๐Ÿ‘‡

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages