WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma Oktoba 23,2021, kuhusu mkakati wa utekelezaji wa sh. bilioni 368 zilizotolewa kwa wizara na Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya Kampeni ya Maendeleo ya Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19. Fedha hizo ni kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu nchini ikiwemo kujenga vyumba vya madarasa 15,000 nchini. Waziri Ndalichako ametoa onyo kwa viongozi watakao jaribu kuchakachua au kufuja fedha hizo na kwamba hawatakuwa tayari kujaribiwa kwa hilo na endapo wakithubutu kufanya hivyo hatosita kuwachukulia hatua kali ikiwemo kuwatimua kazi.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omar Kipanga akizungumza neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri Profesa NdalichakoMdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Waziri Profesa Ndalichako akitoa onyo hilo kwa wote watakaosimamia miradi hiyo.....
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇