BARABARA ZINAZIJENGWA NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
VIONGOZI na wananchi wametoa shukrani kwa Serikali za Awamu ya Sita inayooongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kugharamia ujenzi wa barabara mbalimbali katika jimbo lao la Musoma Vijijini.
A - FEDHA BAJETI 2021/2022
Zimetumika katika ujenzi wa barabara zifuatazo:
(1) Mkirira - Kwangwa Hospital (Gharama: Tsh Milioni 350). Limekamilika kwa 50%
(2) Masinono - Kinyang'erere (Gharama: Tsh Milioni 500). Usanifu wa Madaraja unakamilishwa
(3) Bukima-Bulinga- Bwasi (Gharama: Tsh Milioni 300). Ujenzi umekamilika kwa 80%
B - FEDHA ZA TOZO
(Jumla: Tsh bilioni 2)
Barabara zinatakazojengwa na matayarisho yameanza:
(1) Mmahare-Etaro-Nyasaungu
(2) Mugango-Bwai Kwitururu- Kwikubs
(3) Bwai Kwitururu- Bwai Kumsoma
(4) Maneke-Mayani- Kyawazaru
(5) Nyaminya-Kataryo- Kyawazaru
(6) Rwanga-Seka-Mikuyu
(7) Saragana- Nyambono- Chumwi
(8) Kaburabura-Masinono-Bugwema
(9) Bukima-Bulinga- Bwasi
(10) Busekera-Burungu
(11) Chitare-Kurugee-Buraga (Kivukoni)
(12) Kome - Buira
(13) Kigera Etuma-Ekungu
(14) Nyakatende-Kamguruki- Kigera Etuma
(15) Mkirira-Nyegina-Esira
(16) Kurukerege-Nyegina
WANANCHI:
wanaombwa watoe ushirikiano wa hali ya juu kabisa wakati wa utekelezaji wa ujenzi wa barabara za Vijijini mwetu.
UPATINAKAJI WA MOLAMU:
Wananchi wasaidie MOLAMU ipatikane kwa urahisi ili ujenzi uende kwa kasi.
SHUKRANI:
Jimbo la Musoma Vijiji linatoa SHUKRANI NYINGI sana kwa SERIKALI yetu kwa kutoa FEDHA nyingi za kutekeleza MIRADI ya ujenzi wa barabara Vijijini mwetu. Ahsante sana RAIS wetu, MHE SAMIA SULUHU HASSAN.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijijini
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇