LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 18, 2021

VIKUNDI 325 KUNAFAIKA NA UBORESHAJI KILIMO MUSOMA VIJIJINI




 *UBORESHAJI WA KILIMO NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI*




JIMBO la Musoma Vijijini lenye KATA 21 zenye VIJIJI 68 limeamua KUBORESHA KILIMO chake kwa kufanya yafuatayo:

*Kuunda VIKUNDI vya KILIMO ili kurahisisha upatikanaji wa HUDUMA za KILIMO (k.m. pembejeo, mikopo na ushauri). 

*Kuweka mkazo kwenye Kilimo cha UMWAGILIAJI kwa kutumia Maji ya Ziwa Victoria na maji ya baadhi ya MITO isiyokauka.

*Kuongeza matumizi ya PLAU (jembe la kukokotwa na ng'ombe), na kupunguza matumizi ya JEMBE la MKONO

ORODHA ya Kata 21 na idadi ya Vikundi 362 vya Kilimo kwenye Vijiji vyake 68 ni hii hapa:

*1.KATA YA BUGOJI:* Ina Vijiji 3, Vikundi 13

*2. KATA YA BUGWEMA:* Vijiji 4, Vikundi 14

*3. KATA YA BUKIMA:* Vijiji 3, Vikundi 32

*4. KATA YA BUKUMI:* Vijiji 4, Vikundi 47

*5. KATA YA BULINGA:* Vijiji 3, Vikundi 7

*6. KATA YA BUSAMBARA:* Vijiji 3, Vikundi 9

*7. KATA YA BWASI:* Vijiji 3, Vikundi 9

*8. KATA YA ETARO:* Vijiji 4, Vikundi 21

*9. KATA YA IFULIFU:* Vijiji 3, Vikundi 9

*10. KATA YA KIRIBA:* Vijiji 3, Vikundi 24

*11. KATA YA MAKOJO:* Vijiji 3, Vikundi 27

*12. KATA YA MUGANGO:* Vijiji 3, Vikundi 28

*13. KATA YA MURANGI:* Vijiji 2, Vikundi 7

*14. KATA YA MUSANJA:* Vijiji 3, Vikundi 7

*15. KATA YA NYAKATENDE:* Vijiji 4, Vikundi 12

*16. KATA YA NYAMBONO:* Vijiji 2, Vikundi 6

*17. KATA YA NYAMRANDIRIRA:* Vijiji 5, Vikundi 14

*18. KATA YA NYEGINA:* Vijiji 3, Vikundi 37

*19. KATA YA RUSOLI:* Vijiji 3, Vikundi 5

*20. KATA YA SUGUTI:* Vijiji 4, Vikundi 24

*21. KATA YA TEGERUKA:* Vijiji 3, Vikundi 10

*KILIMO CHA UMWAGILIAJI*

Vijiji vingi vya Jimbo letu viko karibu sana na Ziwa Victoria.  Kwa hiyo, kwa sasa, KILIMO cha UMWAGILIAJI kinawekewa mkazo sana, na WAKULIMA wamekubali kufanya kilimo hiki.

*PAMPU za kumwagilia: baadhi ya VIKUNDI vya KILIMO vilivyoko pembezoni mwa Ziwa Victoria vimejinunulia vyenyewe VIFAA vya UMWAGILIAJI, zikiwemo pampu na mipira ya kumwagilia.

*MFUKO wa JIMBO: Vikundi 15 vilipewa pampu, mipira na mbegu kutoka kwenye Fedha za Mfuko wa Jimbo. 

VIKUNDI hivyo vilitoka KATA za  Bugwema, Bukima, Bukumi, Busambara, Bwasi, Etaro, Kiriba Makojo, Mugango, Murangi, Musanja, Nyakatende, Nyegina, Nyambono na Suguti.

*JEMBE LA KUKOKOTWA NA NG'OMBE (PLAU)*

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini,  Profesa Sospeter Muhongo ameanzisha PROGRAMU ya KUPUNGUZA, kwa kiasi kikubwa, matumizi ya JEMBE la MKONO ndani ya Jimbo lao.

MBUNGE huyo ameishagawa bure PLAU 85 (majembe ya kukokotwa na ng'ombe 85) kwenye VIKUNDI 85 vya KILIMO kutoka Kata zote 21.

Programu hii ni endelevu.

*MAFANIKIO YATOKANAYO NA JITIHADA HIZO KWA WAKULIMA WALIO KWENYE VIKUNDI*

*WANACHAMA wa VIKUNDI vya KILIMO wanasema, kwa sasa mafanikio yao ni pamoja na:

*kupanua mashamba yao kutoka hekari 1 hadi 5 (au zaidi) kwa kila mkulima mdogo. Wanaoendelea kutumia JEMBE la MKONO mashamba yao bado ni madogo madogo.

*kuokoa muda wa kazi shambani kwa kutumia kipindi kifupi kulima kwa kutumia PLAU badala ya JEMBE la MKONO

*baadhi ya VIKUNDI vya KILIMO vimeweza  kugawa mavuno yao ya mazao ya chakula kwenye shule za maeneo yao (chakula shuleni)

*kuongezeka kwa mavuno ya kilimo na mapato ya fedha kwa WANACHAMA wa VIKUNDI vya KILIMO kwa sasa wamepata uwezo wa kusomesha watoto wao ipasavyo, wamefungua biashara mpya, wanakopeshana fedha, na wameweza kujenga nyumba bora.

*OMBI KUTOKA KWA WAKULIMA WA MUSOMA VIJIJINI*

WAKULIMA wa Musoma Vijijini WANATAKA kuelekea kwenye KILIMO cha kutumia MATREKTA. 

Kwenye kipindi hiki cha mpito, wanaomba WADAU wa MAENDELEO, ikiwemo Halmashauri yetu (Musoma DC) waungane na MBUNGE wao wa JIMBO kuwagawia MAJEMBE ya KUKOKOTWA na NG'OMBE (PLAU) ili wapunguze kutumia JEMBE la MKONO.

PICHA zilizoko hapa zinaonesha baadhi ya VIKUNDI vya KILIMO vya Jimbo la Musoma Vijijini vikiwa kazini mashambani mwao.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages