LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 16, 2021

ULEVI WA KUPINDUKIA, WIVU WA MAPENZI VYATAJWA KUONGEZA MATUKIO YA MAUAJI MKOANI KAGERA

Na  Mwandishi Maalum, Kagera.
Jaji Mfawidhi Kanda ya Bukoba, Dk. Ntemi Kilekamajenga, amesema, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba inaweza ikawa inaongoza au ya pili kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji.

Jaji Mfawidhi ameyaeleza hayo jana mbele ya Makatibu Wakuu Watatu waliofika Mahakamani hapo katika  ziara yao ya kikazi ya kujionea shughuli za utoaji hakijinai zinavyotekelezwa katika Mahakama Kuu na Mahakama za Chini mkaoni Kagera, mafanikio na changamoto wanazokabiliana nazo.

Kwa mujibu wa Jaji Mfawidhi Kilekamajenga, ongezeko la kesi za mauaji katika  Mkoa huo  ni suala linalofikirisha si kwa Mahakama peke yake bali pia kwa wadau wengine wanaohusika na mnyororo wa uotaji haki Jinai Mkaoni Kagera.

“Waheshimiwa Makatibu wakuu, kwanza natoa shukrani zangu kwa ujio wenu, haijawahi kutokea  kwa Mahakama yetu kutembelewa na Makatibu Wakuu Watatu kwa wakati moja. Nieleze kwamba moja ya changamoto kubwa tuliyonayo ni idadi kubwa ya kesi za mauaji” Akasema Jaji Mfawishi na  kuongeza;

Anaongeza kwamba, wao kama Majaji na Mahakama  kwa ujumla wamekuwa wakijiuliza sababu za ongezeko la visa hivyo katika Mkoa wa Kagera, Mkoa ambao unapakana  na nchi Jirani tatu, Uganda, Rwanda na Burundi,

“Kanda ya Bukoba inaweza kuwa ya kwanza au ya pili kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji, inafikirisha sana kwa nini kuwa na visa vingi vya mauaji”. Anaeleza Jaji Mfawidhi  Kilekamajenga.

Akasema Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba hadi sasa ina kesi 249 ambazo  zipo tayari kuanza kusikilizwa na kwamba, na kwamba  kesi 49 kati ya  hizo zitaanza kusikilizwa katika kikao maalum cha Mahakama Kuu kitakachoanza Mwezi Novemba Mwaka hu.

Akabainisha kwamba, uendeshaji wa kesi za mauaji pamoja na kwamba zipo complicated lakini zinahitaji  fedha nyingi kuziendesha kulingana na idadi ya mashahidi.
 
Akasema, usikilizaji wa kesi 10, kwa mfano unaweza kugharimu kati ya  shilingi za Kitanzania milioni  20 mpaka 25 kulingana na idadi ya mashahidi hali inayopelekea kusikilizwa kwa kesi chache kutokana na ufunyu wa  bajeti na hivyo  kuathiri mnyororo wa uotaji haki.

“Kesi za mauaji  ni ngumu sana  na zinahitaji  fedha nyingi sana. Tuna  kesi   249 za mauaji, lakini  zitakazoweza kusikilizwa ni 49 tu kutonana na ufinyu wa bajeti, tunaiomba  serikali  ione  namna ya  kusaidia ili  haki iweze kutendeka na kwa wakati na kupunguza msongamano usio wa lazima katika magereza yetu”. Akasisitiza Jaji Mfawidhi Imani Kilekamajenga.

Suala la  kuwapo kwa matukio ya mauaji Mkoani Kagera  halikuelezwa tu na Jaji Mfawidhi wa  Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba bali pia  limezungumwa na   Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa  Bukoba Kamishna Msaidizi  Awadhi Juma Hajji.

Akizungumzia hali hiyo,  RPC  Awadhi Juma Hajji  amesema kwa muda mfupi aliokaa  Mkoani  Kagera,  akiwa ametokeza Zanzibar amekuwa akipokea taarifa za  mauaji  na kubwa linalosababisha  matukio ya kuuana  mkoani  hapa ni  wivu wa mapenzi.

Na kwa sababu hiyo  ameshauri  kuendelea kutolewa kwa elimu kwa jamii  kuacha kujichukulia sheria  mkononi  lakini pia  kila mwananchi katika nafasi yake anapashwa kutimiza wajibu wake ili kupunguza  na kuondoa kabisa matukuo ya  mauaji katika jamii.

“ Muda mfupi ambao nimekaa hapa nimekuwa nikipata taarifa za mauaji hali  si nzuri  sana, wajibu wetu Polisi ni kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao, ninaomba sana ushirikiano kutoka kwa wananchi  na wadau wengine ya Hakijinai, na kila mmoja wetu akitimiza wajibu wetu, changamoto zinazoikabili  jamii zitapungu.Amesisitiza  RPC Hajji.

Naye Mwendesha Mashtaka Mkoa wa  Kagera Juma Masanja akizungumzia  hali hiyo ya mauaji Mkoani  Kagera, licha  ya kusema  visa vingine vinatisha na kushangaza kwamba mwanadamu anaweza kumfanyia hivyo mwanadamu mwenzi amewataka  Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo  kuendelea kutoa elimu kwa wananchi  juu ya  madhara ya kujichukulia sheria mkononi.

“Katika hili  na mimi  naomba nichangie, kwa kweli hali si nzuri, kesi ni nyingi, na wakati mwingine matukio mengine yanatisha na kuogofya mpaka unashangaa hivi ni mtu anaweza kufanya hivi.

Nawaomba Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo mtoe elimu kwa wananchi na muwaeleze kwamba kujichukulia  sheria Mkononi ni Kosa la Jinai” akasitiza Mwendesha Mashtaka Juma Masanja.

Mmomonyoka wa maadili,  watu  kutokuwa na hofu ya mungu, wivu wa mapenzi,  ulevi wa kupindukia, na  migogoro  ya ardhi ambayo nayo imeelezwa kuwa ni mingi  Mkoani  Kagera  ni  baadhi ya sababu zinazoelezwa kuongeza visa ya mauaji katika mkoa huo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu  Wizara ya Katiba  na Sheria, Profesa Sifuni Mchome,  akizungumza visa hivyo, amesema takwimu za matukio hayo zinatisha na  haziendani na  Nchi ambao imeingia katika Uchumi wa Kati.

“Nchi yetu  imeingia katika uchumi wa kati, lakini bado tunafanya mambo  ambayo hayaendani na nchi  iliyoingia katika uchumi wakati, tunapashwa kama jamii kubadilika na ni wazi kuna jambo linatakiwa kufanyika kwa nini jamii imeingia katika hali hii ya  kuuanza” akasisitiza Profesa Mchome.

Makatibu Wakuu Sifuni Mchome ( Katiba na Sheria),  John Jingu ( Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto) na Christopher  Kadio ( Mambo ya Ndani) wamehitimisha ziara yao ya kikazi ya wiki moja katika  mikoa ya Tabora,  Kigoma na Kagera.
///

 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Dkt. Ntemi Kilekamajenga, akielezea  mafanikio na changamoto za utoaji haki jinai katika Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba na Mahakama za chini kwa Makatibu Wakuu watatu  Sifuni Mchome, John Jingu na Chrishopher  Kadio, moja ya  changamoto kubwa aliyoilezea Jaji Mfawidhi ni uwepo wa kesi nyingi za mauaji katika mahakama hiyo, Jumla ya Kesi 249 zimekwisha kamilika upelelezi na 49 kati ya hizo  zitaanza kusikilizwa katika kikao maalum cha Mahakama Kuu kinachotarajiwa kuanza  Mapema Mwezi Novemba mwaka huu.

Majaji wa Mahakama Kuu  Kanda  ya Bukoba, Jaji  Ayubu Mwenda,  Jaji Angaza Mwipopo  na Jaji Emmanuel Ngigwana. Mahakama Kuu  Kanda ya Bukoba ina majaji  wanne (4) pamoja na  kesi nyingi za mauaji, Mahakama Kuu  Kanda ya Bukoba pia inamashauri mengi ya migogoro ya ardhi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages