LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 16, 2021

MAWAKILI WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA TAALUMA ZAO

Na Mwandishi Maalum,  Bukoba
Mawakili wanaotoa  msaada wa kisheria kwa watuhumiwa wa makosa mbalimbali yakiwamo ya jinai, wameshauriwa kutekeleza  jukumu hilo kwa kuzingatia weledi wa taaluma zao na si vinginevyo.

Ushauri huo umetolewa mwishoni mwa wiki na  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria,  Profesa  Sifuni Mchome, katika mazungumzo yake  mafupi na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili  Tanganyika ( TLS) muda mfupi baada ya  Ujumbe wa Makatibu Wakuu wakiongozwa na  Profesa Mchome, kumaliza  mazungumzo yao na  mahabusu na wafungwa  wanaume na  wanawake waliopo katika Gereza la Bukoba.

Wakiwa ndani ya  Gereza hilo upande wa Gereza la Wanawake,  Makatibu wakuu hao  walikumbana na kisa cha mahabusu mmoja ambaye amekaa  ndani ya  gereza hilo kwa zaidi ya miaka sita sasa akisubiri  kukamilika  kwa upepelezi wa tuhuma za mauaji anazokabiliwa nazo.

Mahabusu huyo  aliwaeleza  Makatibu  Wakuu hao, kwamba licha ya yeye kuwa tayari kukili kosa lake na alikuwa tayari kufanya hivyo, lakini  Wakili  aliyekuwa anamsimamia alimkataza kukiri kosa lake kitendo ambacho kimemfanya aendele kusota Gerezani.

Ni kutokana na maelezo ya mahabusu huyo, ndipo  Katibu Mkuu Profesa Mchome anapowataka  mawakili  kuzingatia weledi wa taaluma zao na kuacha kukikua maadili ya kazi zao.

“ Hapana naona kuna shida ya maadili hapa  hakuna jambo jingine “ anasema  Katibu  Mkuu  Mchome,  na kuongeza “Bw. TLS, nikuombe  hebu kaa na  mawakili wako  muliangalie hili, zungumzeni. Kama mtuhumiwa anataka  mwenyewe kwa hiari yake kukili  kosa lake mwacheni afanya hivyo, kwa sababu yeye ndiye anayejua ukweli wa nini alichokifanya, shaurini  vizuri zingatieni maadili ya kazi zenu na   taaluma zenu”. Akasisitiza  Katibu Mkuu  Mchome.

Katibu Mkuu  Mchome,  akaeleza pia kwamba kazi kubwa ya Mawakili na Wanasheria ni kutoa ushauri wa kisheria   kwa weledi, maadili mema, kwa wakati na kufanya kazi kwa matokeo  ili  haki itendeke na  na taifa  liendelee kupiga hatua za  maendeleo.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu  Profesa Mchome amesema, atatuma timu  ya Wanasheria  Kutoka  Wizara ya Katiba na Sheria ili kwenda kutoa msaada wa kisheria  Mkoani Kagera. //

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome, akizungumza na Wakili wa Kujitegemea na   Mwenyekiti wa  Chama cha Mawakili  wa Tanganyika ( TLS) Kanda ya Kagera  Peter Mussa  wakiwa nje ya Gereza la Wanawake Bukoba baada ya kuwatembelea na kufanya mazungumza na  mahabusu na wafungwa  wanawake na wanaume. Katibu Mkuu Mchome alimtaka  Mwenyekiti wa TLS pamoja na  mambo mengine  kuzungumza na  mawakili wenzie umuhimu wa kuzingatia maadili ya taaluma yao wakati wakitekeleza majukumu yao.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages