LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 7, 2021

TAIFA STARS HOI NYUMBANI, YACHAPWA NA BENINI BAO 1-0, UWANJA WA MKAPA DAR ES SALAAM, LEO

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeshindwa kutamba katika Uwanja wake wa nyumbani baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa timu ya Taifa ya Benini katika mchezo wa makundi kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Qatar.

Katika kipindi cha kwanza Taifa stars walicheza vizuri lakini licha kupata nafasi nyingi za kufunga magoli walishindwa kuzitumia nafasi hizo na kuwafanya kwenda mapumziko kila timu ikiwa haikupata kitu.

Kipindi cha pili Timu ya Taifa ya Benini baada ya kufanya mabadiliko ya wachezaji wake kadhaa mabadiliko hayo yalizaa matunda kwani mchezo ulibadilika na kuanza kulisakama lango la timu ya Taifa ya Tanzania na hatimaye kupata bao la kuongoza katika dakika ya 71, kupitia kwa mshambuliaji wake Steven Mounie kwa shuti kali ambalo lilimshinda Aishi Manula na kuingia nyavuni.

Juma lijalo timu hizo zitacheza mchezo wa mwingine wa marudiano ambapo Taifa Stars watawafuata Benin katika uwanja wao.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages