Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Christian Blind Mission (CBM), Nesia Mahenge akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Oktoba kuhusu Wiki ya Asasi za Kiraia nchini (AZAKI) inayotarajia kuanza kesho kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakya Kikwete jijini Dodoma.
Uzinduzi wa wiki hiyo ya AZAKI unatarajiwa kufanywa na Mgeni rasmi Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye pia atakatembelea mabanda ya maonesho ya asasi mbalimbali nje ya ukumbi huo wa mikutano.
Mahenge amesema zaidi ya asasi 150 zimejisajiri kushiriki kwenye wiki hiyo ambayo pia itaambatana na makongamano, Kauli Mbiu ya mwaka huu ni: Mchango wa AZAKI katika Maendeleo ya Tanzania.
Aidha, Mahenge amesema kuwa ili kuhamasisha wananchi kuhudhuria maonesho hayo, wameandaa usafiri wa bure katika maeneo mbalimbali jijini Dodoma wa kuwapeleka kwenye ukumbi na kuwarudisha nyumbani, lakini vilevile kutakuwepo banda maalumu kwa ajili ya watu kwenda kupata chanjo dhidi ya UVIKO-19.
Naye,Mkurugenzi Mtendaji wa Asas ya Umoja wa Mataifa Tanzania UNA-Tanzania, Reynald Maeda amesema kuwa kutakuwepo na makongamano kwa ajili ya kujadiliana mambo mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo mchango wa Azaki katika maendeleo ya Tanzania.
Wanahabari wakiwa katika mkutano huo.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video ujue viongozi hao wa AZAKI wakielezea kuhusu maandalizi ya wiki hiyo...Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇