Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Évariste Ndayishimiye, baada ya mgeni huyo kuwasili katika Viwanja vya Ikulu, Chamwino Jijini Dodoma, leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Évariste Ndayishimiye wakipokea heshima ya nyimbo za Mataifa mawili ya Tanzania na Burundi na wimbo wa Afrika Mashariki wakati zikipigwa wakati Mgnei huyo alipopokewa katika Viwanja vya Ikulu, Chamwino Jijini Dodoma.Rais wa Jamhuri ya Burundi Evariste Ndayishimiye akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) baada ya kupokewa katika viwanja vya Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma leo.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akimtambulisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Évariste Ndayishimiye kwa Viongozi mbalimbali wa Serikali baada ya kupokewa katika viwanja vya Ikulu, Chamwino Jijini Dodoma, leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akizungumza na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Evareste Ndayishimiye , baada ya kumpokea, Ikulu, Chamwino jijini Dodoma, leo.-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongoza Ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo rasmi na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Evariste Ndayishimiye na ujumbe wake, Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma, leo.Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akizungumza kwenye
mkutano na Waandishi wa Habari, Ikulu Jijini Dodoma. Kushoto ni Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Evareste Ndayishimiye.Rais wa Jamhuri ya Burundi Evareste Ndayishimiye akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari, Ikulu Chamwino Jijini Dodoma, leo Oktoba 22, 2021. Kulia ni Rais Samia, akimsikiliza. (Picha zote na Ikulu)
Your Ad Spot
Oct 22, 2021
Home
featured
Kitaifa
RAIS SAMIA AMPOKEA MGENI WAKE RAIS WA BURUNDI ALIYEWASILI NCHINI LEO, WAFANYA MAZUNGUMZO IKULU JIJINI DODOMA
RAIS SAMIA AMPOKEA MGENI WAKE RAIS WA BURUNDI ALIYEWASILI NCHINI LEO, WAFANYA MAZUNGUMZO IKULU JIJINI DODOMA
Tags
featured#
Kitaifa#
Share This
About Bashir Nkoromo
Kitaifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇