LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 4, 2021

RAIS SAMIA AZUNGUMZA KWA NJIA YA MTANDAO NA BOSI WA KAMPUNI YA ROYAL DUTCH SHELL YA UHOLANZI, LEO

Ikulu, Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, leo amezungumza kwa njia ya mtandao na  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Dutch Shell yenye makao yake makuu  nchini Uholanzi, Ben Van Beurden.

Van Beurden amemshukuru Rais Samia na kueleza kuwa wanaridhishwa na jinsi Serikali ya Awamu ya Sita ilivyoboresha mazungumzo ya uwekezaji kwenye mradi wa Gesi asili iliyosindikwa (LNG) hapa nchini.

Kwa upande wake Rais Samia amemshukuru Van Beurden kwa nia yao njema ya kutaka kuwekeza kwenye mradi huo ambao utachochea kukuza uchumi waTanzania.

Kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya mtandao Ikulu Chamwino mkoani Dodoma,  kimehudhuriwa na Waziri wa Nishati January Makamba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Leonard Masanja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dk. James Mataragio.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages