LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 4, 2021

MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM, MAKAMU WA RAIS DK. MPANGO AANZA ZIARA YA KICHAMA MKOA WA DAR ES SALAAM, LEO

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango leo ameanza ziara ya Kichama katika mkoa wa Dar es Salaam.

Katika Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Mpango alipowasili amepokewa na wananchi na Wana CCM, Wajumbe wa Kamati za Siasa za Wilaya zote mkoa huo wakiongozwa Mwenyekiti wa CCM mkoa Kate Kamba na Katibu wa CCM wa mkoa huo Saibu Akwilombe.

Katika ziara hiyo, Dk. Mpango ambaye pia ni Mlezi wa Kichama wa mkoa wa Dar es Salaam, baada ya kutoka Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam, ataenda katika Ukumbi wa Karimjee kuzungumza na Wazee wa mkoa huo.

Kwa mujibu wa ratiba ya awali, kesho Dk. Mpango ataendelea na ziara yake hiyo kwa ambapo asubuhi anatarajiwa kuzungumza na Wanawake katika  Ukumbi wa PTA Hall, katika Viwanja vya  Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba), Barabara ya Kilwa, Temeke.

Baada ya ya Mkutano wake na Wanawake,  saa nane mchana  Dk. Mpango atakutana na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Iddi Nyundo, ulipo Ofisi za Manispaa ya Temeke.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango akisalimiana na Viongozi mbalimbali baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam, kuanza ziara ya Kichama mkoani humo, leo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango akisalimia Viongozi, Wanacch na Wananchi kwa jumla baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam, kuanza ziara ya Kichama mkoani humo, leo. Kushoto ni Katibu wa CCm mkoa wa Dar es Salaam Shaibu Akwilombe na Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Kate Kamba.
Msafara wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango ulipokuwa ukiwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam, leo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages