LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 16, 2021

RAIS SAMIA AHUDHURIA MAADHIMISHO YA JUBILEI YA MIAKA 50 YA HOSPITALI YA KCMC MOSHI, LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akizindua jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Mionzi katika Hospitali ya KCMC Moshi mkoani Kilimanjaro, wakati wa sherehe ya Maadhimisho ya kumbukizi ya Jubile ya Miaka 50 ya Hospitali hiyo leo, Wa pili kulia ni Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dk. Fredrick Shoo, Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dk. Mollel, kushoto ni Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akisoma maelezo baada ya kuzindua jiwe hilo la Msingi Ujenzi wa Jengo la Mionzi katika Hospitali ya KCMC Moshi mkoani Kilimanjaro, leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu Mnara wa kumbukizi ya Maadhimisho ya Jubile ya Miaka 50 ya Hospitali hiyo ya KCMC;
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye Sherehe hiyo ya Kumbukizi ya Maadhimisho ya Jubile ya Miaka 50 ya Hospitali hiyo ya KCMC Moshi Mkoani Kilimanjaroleo.

Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Dk.  Fredrick  Shoo akimkabidhi Tuzo ya Maadhimisho ya Yubile hiyo ya Miaka 50 ya Hospitali yaKCMC Rais Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya waliohudhuria
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Dkt.  Fredrick  Shoo baada ya kuhutubia kwenye Sherehe ya Kumbukizi ya Maadhimisho ya Yubile ya Miaka 50 ya Hospitali ya KCMC Moshi Mkoani Kilimanjaro leo (Picha zote na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages