LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 16, 2021

CCM YAZINDUA RASMI UGAWAJI KADI ZA KIELEKTRONIKI KWA WANACHAMA DODOMA




 

Katibu Wa NEC Organaizesheni na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dkt. Maudline Cyrus Castico amezindua Rasmi Kadi za Kielektroniki za Chama Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma white House 


Dkt. Maudline Castico amekuwa Mgeni Rasmi wa Uzinduzi wa Kadi za Kielektroniki zaidi ya** Elfu arobaini na sita mia saba thelathini na mbili *(46,732)*** za CCM Mkoa wa Dodoma na wilaya zake 7

Katibu wa Nec Organaizesheni Dkt. Castico amesema Lengo la zoezi hili ni Kukisaidia Chama Cha Mapinduzi kupata Takwimu sahihi za Wanachama wake Kwa ngazi zote 

“ Hadi sasa wanachama waliojisajili kwa Mfumo wa Kielektroniki ni zaidi ya M *.1,854,681* ambapo Mkoa wa dodoma waliojisajili ni zaidi ya 127,068 ikiwa una wanachama zaidi ya *616891* ” Dkt. Maudline Castico

Mwisho Dkt. Castico amewashukuru sana wanachama wote wakiongozwa na Makatibu wa Mikoa kwa kuendelea kuonyesha juhudi za kusajili wanachama katika mfumo mpya wa kieletroniki kwa kufanya hivi ni kukiunga Mkono Chama Cha  Mapinduzi na kuhamasisha  zoezi hili kwa Mikoa mingine kukamilisha kwa wakati 

Aidha amemaliza kwa kupongeza Mkoa wa Dodoma kwa kuwa Mfamo mzuri wa mikoa mingine katika zoezi la Kusajili kieletroniki na mikoa mingine iige hatua hii nzuri na kufanya vizuri zaidi ya Mkoa wa Dodoma

*# kaziiendelee*

Imetolewa na:

*IDARA YA ORGANAIZESHENI*
*CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)*


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages