LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 29, 2021

MWONGOZO WA HUDUMA YA CHAKULA SHULENI WAZINDULIWA, WANAFUNZI WATOA YA MOYONI+video

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Dkt  Leonard Akwilapo akikata utepe kwa niaba ya  Waziri wa wizara hiyo, Profesa Joyce Ndalichako ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Mwongozo wa Kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni. Wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu wa Tamisemi, Profesa Riziki Shemdoe (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia (Sayansi), Profesa James Mdoe.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Dkt Leonard Akwilapo  akiwa na  viongozi wengine wakionesha mwongozo huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Dkt Leonard Akwilapo  akimkabidhi mwongozo Katibu Mkuu wa Tamisemi, Shemdoe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Dkt Leonard Akwilapo  akimkabidhi kitabu cha mwongozo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Stanslaus Nyongo.
Mbunge Viti Maalumu ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Neema Lugangira akikabidhiwa mwongozo.
Mkurugenzi Mkaazi wa Taasisi ya PCI, Nicolas Ford akikabidhiwa mwongozo.
Jumanne Sagini Mbunge wa Butiama Mkoa wa Mara ambako mradi wa Lishe shuleni umefanyiwa majaribio na  matokeo kuwa mazuri, akikabidhiwa mwongozo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, akikabidhiwa mwongozo.
Mfano wa vyakula vyenye lishe
Katibu Mkuu Akwilapo akigawa maziwa kwa wanafunzi





Katibu Mkuu Akwilapo  akipata maelezo kutoka kwa  wanafunzi  kuhusu faida ya kupata chakula shuleni na hasara ya kukosa chakula.
Brass Band ya Shule ya ST Home kutoka Buigiri Dodoma, wakitumbuiza wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika hafla ya uzinduzi huo.



 Msanii maarufu wa muziki wa Singeli, Msaga Sumu akitumbuiza kwa wimbo maalumu wa kuhamasisha lishe shuleni.


PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video hapa chini, ujue kilichozungumzwa na wanafunzi kuhusu furaha yao ya kupatiwa chakula shuleni......
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
 Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages