LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 7, 2021

MBUNGE MWANYIKA AKAGUA MRADI WA MAJI WA BIL. 3.9 ALIOUPAMBANIA NJOMBE+video




Mbunge DEO MWANYIKA ametembelea mradi mkubwa wa Maji wa Igongwi  wa Billion 3.9 ambao aliupigania sana ndani ya Bunge - Mh Mbunge akiitaka serikali itenge fedha katika budget ili mradi huu uanze tena baada ya kusimama tangu 2017. 

Serikali ilisikia kilio cha Mbunge Mwanyika na Kutenga fedha na hivyo mwezi wa August 2021 mkandarasi alisaini mkataba Mpya  na sasa Ujenzi umeanza tena.

 Mbunge alitembelea eneo hilo Oktoba 6,2021 aliambatana na ofisa wa Ruwasa kuangalia Utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha unakamilika ndani ya muda kwa kuangalia kama kuna changamoto nyingine ili azishughulikie. 

Mradi huu ambao unachukua maji kutoka kwenye Intake 4 tofauti kwenye Milima ya Madope- Ludewa utawapatia maji safi na salama wananchi wa kata tatu- Matola, Luponde na Uwemba na vijiji zaidi ya Sita. 

Ni maji ya uhakika. Itakumbukwa kwamba Mh Mbunge aliwaahidi wananchi wa kata hizo tatu kwamba atafuatilia na kuhakikisha mradi huo anaukwamua.

 Mh Mbunge vile vile ameshirikiana na Wafanya kazi wa Mkandarasi kuchimba mtaro. Mh Mbunge amemtaka mkandarasi kukamilisha haraka uchimbaji wa mtaro kwa kuongeza nguvu kazi. Vile vile amesisitiza Mabomba ya letwe site haraka.

Mdau, nakuomba uendelee kuona kupitia clip hii ya video hapa chini, Mbunge Mwanyika akitembelea mradi huo....



 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages