Goba, Dar es Salaam
Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayewakilisha Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Mahawanga amezindua vikundi 16 vya wanawake wajasiriamali katika Kata ya Goba, Wilayani Ubungo.
Vikundi hivyo viko chini ya mwavuli wa Goba Women Coporate, vilizinduliwa katika sherehe za Siku ya Wanawake Goba.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Mbunge Janeth , amesema uanzishwaji wa vikundi ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mwito wa Mwenyekiti wa Chama, Rais Samia Suluhu Hassan.
Aliwataka wanake mkoani Dar es Salaam kutumia fursa zilizopo mkoani humo ili kujikwamua kiuchumi.
“Wanawake wa Dar es Salaam ile hali tu ya kuishi hapa Dar ni fursa ya kutosha, kwa sababu tumezungukwa na fursa nyingi ambazo ni rahisi kuzifikia,”amesema Mbunge Mahawanga.
Ameeleza, kiu yake kama mwakilishi wa wanawake Bungeni ni kuona Dar es Salaam, inakuwa ya kwanza kupata matokeo bora katika vikundi.
“Nitumeni niwatumikie.Niiteni na nitakuja tuongee namna ya kujikwamua kiuchumi. Fedha za mikopo isiyo na riba zipo nyingi katika halmshauri zetu, hivyo suala la mitaji siyo changamoto kabisa,”ameeleza Janeth Mahawanga.
Amefafanua pia Rais Samia, ameeleza kuwa Ikulu kuna fedha zinazoweza kukopeshwa kwa njia ya vikundi hivyo ni lazima wanawake kujiunga katika vikundi hivi.
“Tuwaone wataalamu wa maandiko, watuandikie miradi. Tusajili vikundi . Wanawake hatuwezi kupata mafanikio kama ni wavuvi, hatuwezi kujifunza, kutafuta watalaamu na kuwa wazito wa kukopa,”amebainisha Mbunge huyo.
Amehimiza vikundi vya wajasiriamali vya wanawake alivyo zindua na vingine mkoani humo, kudumisha upendo na kuacha kutengeneza matabaka ya walionacho na wasio nacho au wakongwe na wapya.
“Hii inauwa vikundi. Wote jioneni mko sawa. Fuateni katiba ya kikundi. Tupande mbegu mpya ya upendo,”amesema.
Awali mlezi wa Goba Women Coporate, Imgard Mchopa, ameeleza , walianzisha umoja huo miaka saba iliyopita.
“Wazo lilianza mwaka 2014, kutokana na Goba kutishiwa na uhalifu. Wanawake tuliamua kutambuana kwa kujiunga katika kundi moja. Hapo vikazaliwa sasa vikundi vya ujasiriamali,”amesema.
Ameongeza kuwa hadi sasa wana wanachama zaid ya 800 na wamekuwa wakijishughulisha na shughuli mbalimbali za ujasiriamali na wana malengo ya kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo kuchukua tenda za usafi na ulinzi.
“Hata hivyo tunaomba kuwezshwa kupata mikopo ya halmashauri ili tupate mitaji. Kupata elimu ya ujasiriamal na vikundi,”amebainisha.
Mbunge wa Viti Maalum, Janeth Mahawanga (kulia) na Mlezi wa Umoja wa Wanawake wa Kata ya Goba, Imrgard Mchopa wakionyesha Katiba ya Umoja huo, baada ya kuizindua, Dar es Salaam, leo.
Mbunge wa Viti Maalum, Janeth Mahawanga akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇