LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 12, 2021

MASHINDANO YA CAPITAL MARATHON YALIVYORINDIMA DODOMA

Watu mbalimbali wakishiriki mbio za Capital Marathon zilizofanyika eneo la Chuo Kikuu  cha Dodoma (UDOM), jijini Dodoma Oktoba 10,2021, chini ya mdhamini mkuu Shirika la Bima la Taifa (NIC) pamoja na wadhamini wengine. Mgeni rasmi katika mbio hizo alikuwa Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson ambaye pia alishiriki kukimbia.
Mgeni rasmi, Dkt Tulia Ackson (kulia) akimkabidhi zawadi ya sh. milioni  1 msichana Failuna Matanga mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake Km 21.Failuna aliliwakilisha Taifa katika mashindano ya kimataifa ya Marathoni ya Olimpiki nchini Japan na kushika nafasi ya 24.
Ni mbio kwa kwenda mbele
Mmoja wa washiriki wa mbio hizo akivishwa  medali.

Baadhi ya wakimbiaji wakivishwa medali baada ya kumaliza 



Mtangazaji wa Kituo cha Luninga cha  ITV, Shaban Tolle akivishwa medali baada ya kushiriki mbio hizo.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Yesaya Mwakifulefule akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mbio hizo. Mwakifulefule ameahidi NIC kudhamini tena mashindano hayo mwakani.
Mwaandaji wa mashindano hayo ya Capital Marathon, Nsilo Mlozi akishukuru wote waliosaidia kufanikisha mbio hizo.
Dkt Tulia akiwavisha medali baadhi ya washindi wa mbio hizo.





Kikosi kazi cha wafanyakazi wa NIC waliokuwepo kuhakikisha udhamini wa shirika lao unafanikisha  mashindano hayo.

PICHA YOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, Nakuomba uendelee kuona/kusikiliza kupitia clip hii ya video uje yaliyojiri katika mashindano hayo ya mbio ....
 

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages