Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Michuano ya Ligi ya Soka ya Kombe la Mbunge wa Jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam, Dorothy Kilave (Kilave Jimbo Cup 2021) imeanza kutimua vumbi leo baada ya kuzindulwa na Mbunge huyo katika Uwanja wa Sigara (TCC) au Gwambina Longe Chang'ombe.
Akzungumza katika uzinduzi huo, Mbunge Kilave amesema amechukua hatua ya kuanzisha michuano hiyo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa nafasi yake ya Mbunge wa CCM, lakini akasema kwa kuwa ni Mbunge wa Jimbo la Temeke amewahusisha kwenye michuano hiyo wanamichezo wa itikadi zote bila kujali wanatoka vyama gani.
Amesema ni vema Wanamichezo wote kufika kushuhudia michuano hiyo kwa kuwa michezo ni afya lakini pia ni chanzo cha pesa na kuongeza kuwa mwishoni mwa michuano hiyo zitatolewa tuzo mbalimbali kwa washindi na timu na wachezaji bora.
Amesema pia Wakati wa michuano hiyo itakuwa inatolewa chanjo ya Uviko 19, hivyo akawasihi wananchi kujitokeza kupata chanjo hiyo, akisema pamoja na kujikinga lakini pia ni kumuunga mkono Rais samia Suluhu Hassan kwa kuwa yeye alitanguliwa kupata chanjo hiyo.
"Tazameni Rais wetu Mheshimiwa Samia amekwisha chanjwa na anachanja mbuga huku na huko kutumikia Watanzania bila kutetereka. hata mimi mwenyewe nimeshachanjwa kwa hiyo Chanjo hii ni salama, njoo mchanjwe bila hofu yoyote", amesema Mbunge Kilave.
Katika Michuano hiyo Timu ya Kuarasni imeibuka kidedea baada ya kuichapa mabao 2-1 timu ya Buza katika mechi kali ya Ufunguzi iliyopigwa kwenye uwanja huo wa Sigara (TCC) Gwambina, Changombe.
Katika Michuano hyo ya kuwania Kombe la Kilave Jimbo Cup 2021 zinashiriki jumla ya timu 16, 13 kutoka katika Kata 13 za Jimbo la Temeke, na timu nyingine 3 zitatoka katika Taasisi za Vyuo, Kwa Uwakilishi Chuo Cha DUCE, Bandari na T.I.A.
Timu hizo zimepangwa katika makundi kama ifuatavyo;- Kundi A: Temeke, Buza, Yombo vituka na Kurasini. Kundi B: Mtoni, Sandali, DUCE, na Chang'ombe, Kundi C: Tandika, Kilakala, Miburani, T.I.A (Uhasibu) Kundi D: Keko, Bandari, Makangarawe na Azimio.
Hapari katika Picha:
Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave akipiga mkwaju golini kuzindua Michuano ya Ligi ya Soka ya Kilave Jimbo Cup 2021, katika Uwanja wa Sigara (TCC) au Gwambina Longe Chang'ombe, leo.Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave akizungumza wakati wa kuzindua Michuano ya Ligi ya Soka ya Kilave Jimbo Cup 2021, katika Uwanja wa Sigara (TCC) au Gwambina Longe Chang'ombe, leo.Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave akitambulishwa kwa Wachezaji wa timu ya Buza wakati wa uzinduzi wa Michuano ya Ligi ya Soka ya Kilave Jimbo Cup 2021, katika Uwanja wa Sigara (TCC) au Gwambina Longe Chang'ombe, leo.Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave akitambulishwa kwa Wachezaji wa timu ya Kurasini wakati wa uzinduzi wa Michuano ya Ligi ya Soka ya Kilave Jimbo Cup 2021, katika Uwanja wa Sigara (TCC) au Gwambina Longe Chang'ombe, leo.Kikosi cha Timu ya Buza kilichomenyana na Kurasini
Kikosi cha Kurasini kilichomenyana na Buza.
Mtanange ulivyokuwa kwa ufupi👇
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇