LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 7, 2021

KILAVE JIMBO CUP 2021 KUANZA KURINDIMA OKTOBA 17, KWA KUVAANA BUZA NA KURASINI KATIKA MECHI YA UFUNGUZI

Na Mwandishi wa CCM Blog
Ligi ya Soka ya Kombe la Mbunge wa Jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam, Dorothy Kilave linatarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 17, 2021, kwa timu ya Kata ya Buza kumenyana na Kurasini katika uwanja wa Sigara (TCC) Gwambina, Changombe.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge huyo, imesema, katika maandalizi ya michuano hiyo, Dorothy Kilave ameongoza kikao cha ufunguzi wa Ligi ya Kombe la Mbunge Jimbo la Temeke, kikao hicho kikihudhuriwa na Madiwani wa Kata zote 13, za Jimbo la Temeke, Kamati ya Maandalizi ya Kombe la Mbunge inayo ongozwa na Ally Semnyau, Viongozi wa Mpira wa Miguu Temeke (TEFA) Wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa Allex Rwambano na Afisa Michezo wa Manispaa ya Temeke Kimario,

Kwa mujibu wa Ofisi ya Mbunge huyo, pi kikao hicho kimehudhuriwa na Mwakilishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya Wilaya kutoka Jumuiya ya Vijana ambaye ni Katibu wa Vijana CCM Wilaya ya Temeke Endrew Gwaje.

Kombe hilo la Mbunge Jimbo la Temeke, litajumuisha timu 16, 13 zitatoka katika Kata 13 za Jimbo la Temeke, na timu nyingine 3 zitatoka katika Taasisi za Vyuo, Kwa  Uwakilishi Chuo Cha DUCE, BANDARI NA T.I.A Zitashiriki ili kukamilisha timu 16.

Kutoka na zoezi la upangaji wa Timu zote katika ushiriki, Makundi yamepatikana kama ifuatavyo:
Kundi A: Temeke, Buza, Yombo vituka na Kurasini. Kundi B: Mtoni, Sandali, DUCE, na Chang'ombe, Kundi C: Tandika, Kilakala, Miburani, T.I.A (Uhasibu) Kundi D: Keko, Bandari, Makangarawe na Azimio.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Mbunge Kilave, Kamati ya Uratibu wa Mashindano imejipanga Vyema katika kufanikisha Jambo hili kwa Ufanisi na kukidhi kiu za wapenzi wa Mpira Jimbo la Temeke.

Kikao cha maandalizi ya Michuano hiyo cha Mbunge Dorothy Kilave na wadau mbalimbali leo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages