LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 7, 2021

DKT YONAZI AFUNGUA SEMINA KWA WATOA HUDUMA WA POSTA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Jim JonazI  akizungumza alipokuwa akifungua semina kwa watoa huduma za Posta ikiwa ni mwendelezo wa Maadhimisho ya Wiki  ya Posta Duniani jijini Dodoma leo Oktoba 7,2021.   la Posta Tanzania (TPC) imezindua Duka la Posta Mtandaoni ambapo inashirikiana  na  maduka 670 duniani. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Baadhi ya watoa huduma wakisikiliza kwa makini wakati Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt Yonaz  akifungua semina hiyo.











 Na Ramadhan Hassan,Dodoma

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya  Habari,Mawasiliano na Teknolojia yaHabari,Dk.Jim Yonazi amewapa maagizo matatu   watoa huduma za posta
ikiwemo  kuleta ubunifu nini cha kufanya ili kuboresha huduma za posta
nchini

Maagizo mengine ni kuwa mabalozi wazuri wa sekta ya posta pamoja na
kupeleka mapendekezo ya kile  ambacho kimefanyika katika sekta hiyo.

Akizungumza leo Oktoba 7,2021,Jijini Dodoma wakati akifungua warsha ya
watoa huduma za Posta,Naibu Katibu Mkuu huyo amesema mkutano huo ni
muhimu hivyo amewapa maagizo ya kuleta ubunifu nini cha kufanya ili
kuboresha huduma za posta nchini

Pia ameyataja Maagizo mengine ni kuwa mabalozi wazuri wa sekta ya
posta pamoja na kupeleka mapendekezo ya kile  ambacho kimefanyika
katika sekta hiyo.

“Posta ni sekta muhimu sana inawezesha bidhaa moja kutoka sehemu moja
mpaka nyingine na usafirishaji wa mizigo bado unabaki kuwa ni kitu
muhimu Serikali imefanya jitihada kubwa na imewekeza kuhakikisha
miundombinu inakuwa rafiki.

“Na  tumeweka Postikodi katika Halmashauri 21 na mipango inaendelea
kuendelea kuweka katika maeneo mengine hii itasaidia mizigo kufika
kila mahali,”amesema.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) Dk.Jabir Bakari amesema warsha hiyo ni muhimu kwani watoa
huduma hao wamekuwa wakitoa huduma ya kusafirisha mizigo kutoka eneo
moja mpaka jingine.

Amesema kwa kutumia mkutano huo watajadiliana ni changamoto zipi
wamekuwa wakikutana nazo na kisha kuzitafutia ufumbuzi.

“Pia tupo hapa kuona teknolojia inatusaidiaje kutoka katika hili wimbi
la Uviko 19 kwa kuongeza ufanisi katika eneo la posta.Tupo katika
mwelekeo mzuri kutumia sekta ya posta tunatembea vizuri tunataka
kuongeza kasi zaidi,”amesema.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages