Mwanamuziki nguli wa Taarab Khadija Kopa akichangamsha ukumbi kwa kuimba wimbo wa kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mwanamke mchapakazi, huku akiwa amezungukwa na Kina Mama wenye nyuso za furaha, kabla ya Hafla ya uzinduzi wa Chama cha Wanawake Wakandarasi Tanzania, kuanza,
Mgeni Rasmi Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof, Makame Mbarawa (Wapili kulia) akiwa amesimama na viongozi wa meza Kuu baada ya kuwasili ukumbini kuzindua Chama cha Wanawake Wakandarasi Tanzania. Uzinduzi ambao aliufanya kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan. Kushoto ni RAS wa mkoa wa Dar es Salaam Hassan Lungwa na Rais wa chama hicho Judith Odunga na kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), Ofisi ya Afrika Mashariki Wellington Chibebe.Mshauri na Mlezi wa TWCA Balozi Getrude Mangela akiwa ameungana na wengine kusimama wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa mwanzoni mwa hafla hiyo. Wapili kulia ni Mjumbe wa kamati ya Maandalizi ya Hafla hiyo Mhandisi Kulthum Sagamiko ambaye pia ni Diwani Mstaafu Msasani kwa tiketi ya CCM.
Waalikwa wakiwa wamesimama wakati ukipigwa wimbo huo wa Taifa.
Mshauri na Mlezi wa TWCA Balozi Dk. Getrude Ibengwe Mongela akimwelekeza jambo Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Hafla hiyo Mhandisi Kulthum Sagamiko wakati wa hafla hiyo.Ukht Mariam akiongoza Dua ya Kiislam mwanzoni mwa hafla hiyo.
Mchungaji Winnie Kileo akiongoza Maombi ya Kikristo kabla ya kuanza hafla hiyo.
Washiriki wakiwa wamesimama wakati wa maombi hayo ya Kikristo.
Mhandisi Dk. Christina Kayoza akifanya Utambulisho wa wageni waalikwa mwanzoni wa hafla hiyo.
Rais wa TWCA Rais Judith Odunga akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo pia alimkaribisha Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), Ofisi ya Afrika Mashariki Wellington Chibebe akizungumza katika hafla hiyo.
Mshauri na Mlezi wa TWCA Balozi Dk. Getrude Mongela akizungumza katika hafla hiyo. Balozi Mngela aliwafunda wanawake kwamba wakati wa kulalamika umeshapita, sasa ni wakati wa kuchapa kazi. "Tafsiri ya Usawa lazima iwe stahiki, siyo ili mradi kuwa sawa tu, lazima katika kutafuta usawa siyo kuwa sawa tu na mwanaume bali mwanaume milionea", akasama Dk. Mongela.
Washiriki na wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
RAS wa mkoa wa Dar es Salaam Hassan Lungwa akizungumza katika hafla hiyo. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa, akihutubia kabla ya kuzindua Chama Cha Wanawake Makandarasi Tanzania (TWCA) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, jana.Baadhi ya Viongozi Mashuhuri wakiwa kwenye hafla hiyo
Baadhi ya Waalikwa na Washiriki wakiwa kwenye hafla hiyo
Rais wa TWCA akimpongeza Waziri Prof Mbarawa baada ya hotuba yake kwenye hafla hiyo.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa, akikata utepe kuzindua Chama cha TWCA, baada ya kuhutubia Rais wa TWCA akimkabidhi Waziri Mbarwa baadhi ya nyaraka za Chama hicho Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) Mhandisi Consolata Mgimbwa akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Vcky Kamata akitumbuiza wimbo wa 'Wanawake na Maendeleo", kuchangamsha ukumbi wakati wa hafla hiyo.
Viongozi na Wajumbe wa TWCA na waalikwa akiselebuka kucheza wimbo huo wa Vicky Kamata.
Rais wa TWCA Judith Udunga akimkabidhi tuzo ya TWCA Waziri Mbarawa
Waziri Mbarawa akimkabidhi tuzo ya TWCA Rais wa Chama hicho Judith Odunga.
Waziri Mbarawa akimkabidhi tuzo ya TWCA Balozi Dk. Mongela.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa na viongozi wengine wa meza kuu wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Hafla hiyo ya uzinduzi wa Chama cha Wanawake Makandarasi Tanzania (TWCA), mwishoni mwa hafla hiyo, jana. HONGERA TWCA
©2021 CCM Blog/Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇