LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 29, 2021

WAZIRI KIJAJI: ALAT FEDHA ZIPO ZA KUTOSHA TEKELEZENI HARAKA MFUMO WA ANUANI ZA MAKAZI

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza alipokuwa akifungua semina ya kuwajengea uelewa na kuhamasisha utekelezaji  wa mfumo wa Anuani za Makazi kwa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) jijini Dodoma Septemba 29,2021

.Dkt  Kijaji amewathibitishia wajumbe kuwa zaidi ya sh. bilioni 40 zimetengwa katika wizara hiyo kwa ajili ya kutekeleza mpango huo wa Anuani za Makazi lakini pia katika wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Ofisi ya Rais (TAMISEMI) kuna fedha zimetengwa kwa ajili hiyo.

Amewaomba wajumbe wa ALAT kila eneo walipo waunganishe nguvu kusaidia kuutekeleza haraka mfumo huo wa Anuani za Makazi ili ifikapo mwaka 2025 uwe umekamilika katika ngazi zote nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula akizungumza neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri Dkt Kijaji wakati wa semina  huo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange aki
zungumza kuhusu umuhimu wa Anuani za Makazi na jinsi wizara hiyo ilivyojipanga kuutekeleza katika Halmashauri zote nchini..
Mwenyekiti wa ALAT, Yusuf Ngeza akielezea jinsi alivyonusurika kukosa  kuingia mkataba wa kimataifa wa kibiashara kwa kutokuwa na Anuani ya Makazi

 

Wabunge wajumbe wa ALAT wakifanya kikao chao  baada ya semina hiyo. kumalizika
Mbunge wa Kishapu, Boniface Butondo (kulia) akiwa miongoni mwa  wajumbe wa ALAT.



Mbunge wa Butiama ambaye pia ni Mjumbe wa ALAT, Jumanne Sagini akielezea umuhimu wa Mfumo wa Anuani ya Makazi na kuwataka wajumbe wenzie kwenda kuutekeleza ili kurahisisha mawasiliano nchini.
Mbunge wa Ulyanhulu,  Rehema Migilla akiuliza maswali pamoja na kutoa ushauri jinsi ya kuuboresha mfumo huo wa Anuani za Makazi kwa kutumia mfumo wa kitanzania badala ya Google.
Baadhi ya wajumbe wa ALAT wakisikilza kwa makini wakati wa semina hiyo.
Mkurugenzi wa zamani wa Jiji la Mwanza, ambaye sasa ni amehamishiwa  Nzega, Kiomoni Kibambo akielezea jinsi alivyofanikisha mfumo wa Anuani za Makazi katika jiji hilo na kuwa mfano wa kuigwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Geita, Zahara Michuzi  (kushoto) akiwa miongoni mwa wajumbe wa ALAT waliohudhuria semina hiyo muhimu.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara hyo,Injinia Clarence Chwekeleza  akielezea jinsi wizara ilivyojipanga kuutekeleza mfumo huo wa Anuani za Makazi nchini.
Waziri Dkt Kijaji akiagana na wajumbe wa ALAT baada ya kuifungua semina hiyo.
Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe akitoa maoni yake kwamba wakati wa kutekeleza mfumo huo wa Anuani za Makazi halmashauri ziwe makini kupanga vizuri majina ya mitaa ili yasirudiwe rudiwe.



Baadhi ya wajumbe wakitambulishwa  wakati wa semina hiyo.

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA






No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages