LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 20, 2021

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI, LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu
Hassan, amemteua Yona Killagane kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) na pia amemteua Mathew Modest Kirama kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma (PSC).

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu jaffar Haniu imesema, kabla ya uteuzi huu. Kirama alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma (DE), Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kwamba anachukua nafasi ya Nyakimura Mathias Muhoji ambaye amestaafu.

Taarifa imesema Uteuzi huo wa hao wote umeanza juzi, Septemba18, 2021

Rais Samia Suluhu Hassan

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages