Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuenzi utamaduni ikiwa ni pamoja na utamaduni wa ngoma za asili kwa sababu Serikali yake ya Awamu ya Sita inatambua matamasha hayo.
Amesema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi katika Tamasha la Ngoma za Asili lijulikanalo kama Tulia Traditional Dances lililofanyika katika Viwanja vya Uwanja wa Ndege wa zamani jijini Mbeya.
Masanja amesema, Sekta ya Utalii inatambua kwa asilia mia kwamba utamaduni wa ngoma za asili ni sehemu mojawapo ya kuhamasisha utalii na pia unasaidia kuongeza pato la Taifa na pato la mwananchi mmoja mmoja.
Aidha, amewahamasisha wananchi kuendelea kuandaa matamasha kama hayo kwa kila kanda ili mwisho wa siku yavutie wageni kutoka nje ya nchi waje kuangalia utamaduni huo.
Masanja amepongeza Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kwa kurudisha tamasha la Utamaduni wa ngoma.
Your Ad Spot
Sep 24, 2021
NAIBU WAZIRI MARY MASANJA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUENZI UTAMADUNI WA ASILI
Tags
featured#
Sanaa#
Share This
About Bashir Nkoromo
Sanaa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇