LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 24, 2021

MTAA KWA MTAA NA MHE. JANETH MAHAWANGA

Alhamis, Sept 23,2021

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janeth Mahawanga ameunga mkono kampeni ya Mtaa kwa Mtaa inayoendeshwa na kituo cha Redio cha Rise and  shine 98.5AM24 Radio, yenye dhamira ya kusaidia wanawake wanaofanya vyema mtaani.

katika kampeni hiyo Mhe Janeth Mahawanga kupitia Taasisi yake ya Tisha Mama Foundation amewaunga mkono kwa kudhamini zawadi kwa wanawake watakaoshinda  mitaa yote ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam ambapo zawadi hizo hutolewa mara moja kwa wiki yaani kila Alhamisi, kwa kuanzia alitoa zawadi kwa mshindi wa leo katika viwanja vya Mbagala Zakheim.

Vile vile Mh. Janeth amewapongeza kituo cha  Radio cha Rise and Shine kwa juhudi kubwa wanayofanya kuwafikia akina mama lishe wachanga mitaani  lakini amewaomba kwa kushirikiana naye waweke utaratibu mzuri wa kuwafikia akina mama wa makundi mbalimbali ambao wanapambana kutimiza ndoto zao kama vile wajasiriamali wanaouza bidhaa ndogo ndogo, mboga mboga, matunda na wanaogonga kokoto kwa kuwatia moyo, kuwaunga mkono na  kuwafikia kwa kuwapa elimu ya kuwa katika vikundi ili wanufaike na fursa za mikopo.

Aidha amesisitiza kuendelea kumuunga mkono Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kupitia msisitizo wake juu ya  wanawake kuhakikisha wanajiunga na vikundi Rasmi ili kuweza kupata mikopo ambayo itawasaidia kujikwamua  kiuchumi.





No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages