MBUNGE Joseph Kamonga akiongozana na makuli alipokuwa akikagua ghala la mahindi la Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula (NFRA) Mlangali, ambapo zimehifadhiwa tani 9770 zilizonunuliwa wilayani humo. Kamonga ameiomba Serikali kununua ziada ya mahindi tani 16,000 ambazo had sasa zimo majumbani kwa wakulima..
Mbunge Kamonga akizungumza na baadhi ya wakulima.
Baadhi ya wakulima wakisikiliza baada ya Mbunge Kamonga kumpigia simu Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ili kupata ufumbuzi wa changamoto hiyo.
Msimamizi wa Kituo cha Ununuzi wa Mahindi cha NRFA, Mlangali. Hosea Mathias Mkalama.
Na Richard Mwaikenda, Ludewa
MBUNGE Joseph Kamonga ameungana na wakulima wa jimbo la Ludewa, mkoani Njombe, kuokoa jahazi ili Serikali inunue ziada ya mahindi tani 16,000.
Mbunge huyo ambaye baada ya kuona simu za wakulima zimezidi kuhusu Kilio hicho, aliamua kuacha vikao vya Bunge na kwenda jimboni kujionea uhalisia na jinsi ya kutatua haraka changamoto hiyo.
Alisafiri usiku kucha ambapo asubuhi saa 2 aliwasili Mlangali kilipo kituo pekee wilayani humo cha kununulia mazao cha Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula (NRFA), alikuta baadhi ya wananchi wakimsubiri ili asaidie kutatua changamoto hiyo.
Baada ya kusalimiana nao alikwenda moja kwa moja ofisini kwa msimamizi wa kituo kupata taarifa, ambapo aliambiwa kuwa katika wilaya hiyo wamepangiwa kununua tani 1000 tu za mahindi kwa bei ya sh. 430 kwa kilo badala ya sh 500 iliyotangazwa awali na Serikali na kwamba sh. 70 hukatwa kwa ajili gharama ya kusafirisha kutoka kituo hicho hadi ghala la NFRA lililopo Makambako, kitendo ambacho kilimsikitisha Mbunge.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia clip hii ya video usikilize kilio cha Mbunge Kamonga, wakulima na majibu kutoka kwa msimamizi wa kituo cha NRFA......
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇