Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT), Dk. Philis Nyimbi ametoa pongezi kwa Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa Mwanamke wa kwanza Tanzania kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN).
Pia Dk. Nyimbi amempongeza Rais Samia kwa hotuba nzuri aliyoitoa jana katika Mkutano wa Baraza hilo wa 76 (UNGA76) Jijini New York, Marekani.
Pongezi hizo ambazo amesema amezitoa kwa niaba ya Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Jumuiya hiyo Dk. Nyimbi amesema wanawake wa Tanzania, wamefurahishwa na Hotuba yake nzuri iliyobeba dhamira ya kuboresha uhusiano kati ya Tanzania na Mataifa mengine duniani,
Anesema pia hotuba hiyo imebeba dhamira ya dhati ya Rais Samia katika mapambano ya pamoja dhidi ya UVIKO-19, Ushirikiano katika Shughuli za Uchumi pamoja na Usawa wa Kijinsia.
"HakikaRais Samia anaendelea kuuthibitishia ulimwengu kuwa, wanawake wana uwezo mkubwa wa kushika nafasi kubwa za uongozi na nafasi kubwa za maamuzi", alisema Dk. Nyimbi mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dodoma, jana.
©2021 CCM Blog
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇