Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Yustino Ndugai (Mb), amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mbunge wa Ngorongoro na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (uwekezaji), Mhe. William Tate Ole Nasha kilichotokea tarehe 27 Septemba, 2021 nyumbani kwake Jijini Dodoma.
“Natoa pole kwa familia ya marehemu, Serikali, wananchi wa jimbo la Ngorongoro, Wabunge wote, ndugu na jamaa wa marehemu kwa msiba huu mkubwa.
Mwenyezi Mungu awape nguvu na Moyo wa ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu” amesema Mhe. Spika.
Ofisi ya Bunge inafanya mawasiliano na Serikali kuhusu tarat ibu za mazishi na taarifa zaidi zitatolewa.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe
Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge, DODOMA. 28 Septemba, 2021.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇