Muonekano wa shule ya Sekondari Elimu Maalum Patandi,iliyojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia. |
Mkuu wa Chuo cha Ualimu wa Elimu Maalum Patandi Bw.Luciana Segesela,akiwasilisha taarifa kuhusu ukarabati wa chuo hicho, Ununuzi/ugawaji wa vifaa mbalimbali pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari Patandi Maalum kwa ajili ya uboreshaji wa Elimu nchini kwa Waandishi wa Habari waliofika Chuoni hapo katika ziara ya kuangalia maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho.
Wanafunzi wa Chuoa
cha Ualimu wa Elimu Maalum Patandi wakimsikiliza Mkuu wa Chuo hicho
Luciana Segesela,akiwasilisha taarifa kwa Waandishi wa Habari waliofika
Chuoni hapo katika ziara ya kuangalia maboresho yaliyofanywa na Wizara
ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho kuhusu ukarabati wa
chuo hicho, Ununuzi/ugawaji wa vifaa mbalimbali pamoja na ujenzi wa
Shule ya Sekondari Patandi Maalum kwa ajili ya uboreshaji wa Elimu
nchini
Baadhi ya waandishi
wa habari na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Chuoa cha Ualimu
wa Elimu Maalum Patandi Luciana Segesela,wakati akiwasilisha taarifa kwa
Waandishi wa Habari waliofika Chuoni hapo katika ziara ya kuangalia
maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika
chuo hicho kuhusu ukarabati wa chuo hicho, Ununuzi/ugawaji wa vifaa
mbalimbali pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari Patandi Maalum kwa
ajili ya uboreshaji wa Elimu nchini
Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu wa Elimu Maalum Patandi wakiimba wimbo maalum.
Mkuu wa Chuo cha
Ualimu wa Elimu Maalum Patandi Bw.Luciana Segesela,akionyesha miradi
mbalimbali iliyotekelezwa katika chuo hicho kwa Waandishi wa Habari
waliofika Chuoni hapo katika ziara ya kuangalia maboresho yaliyofanywa
na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho.
Mratibu Taaluma Chuo
cha Ualimu wa Elimu Maalum Patandi Lucas Nkivuyo,akitoa maelezo kuhusu
mashine zinazotumika kwa wanafunzi wasio na usikivu kwa Waandishi wa
Habari waliofika Chuoni hapo katika ziara ya kuangalia maboresho
yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo hicho.
Mwanachuo wa Mwaka wa
Pili idara ya wasioona Amour Athumani mwenye ulemavu wa kutosikia
akionyesha kifaa wanachotumia katika kuwasiliana na kujisome
vilivyotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia
katika chuo hicho.
Mkuu wa Chuo cha
Ualimu wa Elimu Maalum Patandi Bw.Luciana Segesela,akiwa na Waandishi
wa Habari wakiendelea na kukagua miradi mbalimbali iliyotekelezwa na
Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika chuo
hicho.
Wanafunzi wa Chuo cha
Ualimu wa Elimu Maalum Patandi wakiwa katika chumba cha Computer
wakijisomea mara baada ya kupokea vifaa bora kabisa kutoka Wizara ya
Elimu,Sayansi na Teknolojia.
Wanafunzi wa Chuo cha
Ualimu wa Elimu Maalum Patandi wakiwa katika chumba cha Maktaba
wakijisomea mara baada ya ukarabati pamoja na kuletewa vifaa mbalimbali
katika chuo hicho na Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na
Teknolojia.
Ujenzi wa jengo la Maabara ya Sayari ukiendelea.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la Maktaba.
……………………………………………………………………………..
Na Alex Sonna,Arusha
CHUO cha Ualimu wa
Elimu Maalum Patandi Mkoani Arusha kimeelezea mafaniko 15 ambayo
imeyapata mara baada ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kufanya
ukarabati mkubwa katika chuo hicho ikiwemo kuleta mabadiliko chanya kwa
kuongeza fursa na kuinua ubora wa elimu.
Akiongea na Waandishi
wa Habari waliotembelea chuoni hapo kuona miradi inayotekelezwa na
Taasisi hiyo,Mkuu wa Chuo cha Ualimu Maalum Patandi,Luciana Segesela
amesema maboresho yaliofanywa na serikali katika sekta ya elimu kupitia
Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia hususani kwenye vyuo vya Ualimu
yameleta mabadiliko chanya kwa kuongeza fursa na kuinua ubora wa elimu.
Vilevile amesema imesadia kuongeza morali ya kazi kwa wafanyakazi kutokana na kufanyia kazi katika mazingira rafiki na salama.
Pia,amesema imesaidia
uwepo wa utoaji wa elimu bora na kuongeza ufaulu katika mitihani kwani
chuo hicho kimepata ufaulu wa juu na hakunamwanachuo aliyefeli katika
mtihani wa taifa.
“Imeongeza uwezo wa
chuo wa kudahili wanachuo kutoka idadi ya wanachuo 260 hadi
450.Imeendelea kuongeza ari ya ujifunzaji kwa wanafunzi kupitia uwepo wa
vifaa mbalimbali vya kujifunzia ikiwepo vitabu. Tuna Imani hata majengo
ya makataba na maabara yanayojengwa yakiisha yataweza kuchochea zaidi
ari hii ya ujifunzaji kwa wanachuo na wanafunzi,”amesema Segesela
Aidha ameongeza
kuwa ujenzi wa shule ya sekondari ya wenye mahitaji maalumu umeleta
ukombozi na matumaini makubwa kwa Chuo hicho kwani walimu tarajali
wamepata sehemu ya kufanyia mafunzo kwa vitendo
“shule hii inaendelea
kutoa fursa chuoni kwa wakufunzi na wanachuo kufanya tafiti mbalimbali
na kutekeleza mafunzo kwa vitendo kulingana na masomo na idara zao kila
inapohitajika” amesema Segesela
Amesema kuwa
ukarabati na ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia umesaidia
chuo kuweza kuandaa wanachuo wanaoendana na stadi za karne ya ishirini
na moja na mapinduzi ya viwanda ya awamu ya nne kwa kupitia uwepo vifaa
mbalimbali vya ufundishaji na ujifunzaji vilivyoletwa ikiwa ni pamoja na
kusaidia ufundishaji wa TEHAMA kwa kutumia komputa tulizopata na
mafunzo waliyopata wakufunzi.
Vilevile,imeondoa
changamoto kwa wanachuo na watumishi wenye mahitaji maalumu ya kutembea
kutoka eneo moja kwenda jingine kutokana na kuwepo kwa mazingira rafiki
kwao kupitia ujenzi wa njia za kutembelea kwa paving blocks.
“Kuwepo kwa huduma ya
uhakika ya maji safi kupitia uchimbaji wa kisima kirefu cha maji
ambacho kimetatua changamoto kubwa ya tatizo la muda mrefu la maji
chuoni na sekondari,”amesema
Pia,Uwepo wa usafiri
wa ukakika umesaidia kurahisisha utekelezaji wa shughuli za chuo na
huduma kwa wanachuo ikiwemo kuwapeleka wagonjwa hospitalini.
“Chuo kimeongeza
fursa ya mahusiano na taasisi zingine pamoja na mamlaka za serikali ya
wilaya na mkoa kwa chuo kuwezesha kufanikisha shughuli zao mbalimbali
kwa kutumia miundombinu na vifaa vya chuo.
Aidha,Patandi imekuwa
kitovu cha kujifunza kutoka kwa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya
nchi kuhusu masuala mbalimbali ya watu wenye mahitaji maalumu na namna
ya utoaji wa huduma rafiki kwao.
“Kuboresha madhari na
mazingira ya chuo kwani chuo kinaonekana kipya.Ujenzi wa uzio wa chuo
umesaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mali na wanajumuiya ya chuo
Pamoja na kudhibiti suala la nidhamu ya wanachuo kwa kudhibiti
utoro,”amesema.
ZAIDI YA BILIONI 1.1 ZAKARABATI MIUNDOMBINU PATANDI
Katika hatua
nyingine,Mkuu huyo wa Chuo amesema zaidi ya shilingi bilioni moja
zimetumika kukarabati madarasa,mabweni,bwalo,jengo la utawala,mifumo ya
umeme,pamoja na kuboresha maabara ya upimaji wa watoto wenye mahitaji
maalum,katika Chuo cha Ualimu elimu maalum Patandi Mkoani Arusha.
Amesema serikali
kupitia wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imekuwa ikikifanyia
ukarabati chuo kwa awamu tofauti tofauti pamoja na kuongeza miundombinu
mingine ya chuo ili kukidhi mahitaji.
Mkuu huyo wa Chuo
amesema ukarabati huo ni wa madarasa,mabweni,Ujenzi wa njia za
kutembelea kwa paving blocks,Ukarabati wa bwalo na jiko la chuo,Ujenzi
wa choo kipya cha wanaume chenye matundu 15 Na mabafu 15,Ukamilishaji wa
ujenzi wa uzio wa chuo Pamoja na geti lake.
Vilevile,ukarabati wa
jengo la utawala linalotumika sasa,ujenzi wa jingo jipya la utawala wa
chuo,ukarabati wa mifumo yote ya umeme,mifumo ya zamani na ujenzi wa
mifumo mipya ya maji safi na maji taka,kuboresha maabara ya upimaji wa
Watoto wenye mahitaji maalumu.
“Thamani ya ukarabati
huu, kwa ujumla wake pamoja na shughuli zinazoendelea kumaliziwa sasa
ni jumla ya gharama ya shilingi bilioni 1,171,157,613.29,”amesema Mkuu
huyo wa Chuo.
MWAKA 2013-2014 ILITOA BILIONI 1.6
Amesema kwa mfano
mwaka 2013/2014 Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia iliboresha
miundombinu ya chuo kwa kujenga mabweni mawili mapya, kuchimba kisima
cha maji pamoja na kujenga sehemu ya uzio wa chuo kwa gharama ya zaidi
ya shilingi bilioni 1.6,Mradi ambao ulitekelezwa na Mkandarasi Suma JKT.
“Kuanzia mwaka 2017
mwishoni wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imefanya jitihada kubwa
kukarabati na kuboreshaa miundombinu ya chuo ambayo kwa ujumla wake
ukarabati huo umekifanya chuo cha Patandi kuonekana kipya kabisa na
hivyo kuwa na mazingira mazuri ya ufundishaji na ujifunzaji.
“Kwa sasa chuo
kinaendelea na utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa chuo kwa
kushughulikia miundombinu ifuatayo,Kumalizia ujenzi wa jengo la utawala
wa chuo, Kumalizia ujenzi wa njia za kutembelea kwa miguu kuelekea
mabwenini kwa paving blocks,”amesema.
Vilevile,kujenga
maktaba yenye huduma za TEHEMA ndani yake yenye uwezo wa kupokea
wanachuo zaidi ya 250,Kujenga maabara ya sayansi ya masomo ya kemia na
bailojia
“Kwa ujumla Shughuli
zote hizi za ukarabati wa chuo zimetekelezwa kwamfumo wa Force Account
chini ya usimamizi wa washauri elekezi kutoka huo Kikuu cha Sayansi cha
Mbeya (MUST),”amesema.
Amesema Chuo hicho
kina wanafunzi wa mwaka wa pili 175 (me-84 na Ke-91) na wanachuo wa
mwaka wa kwanza waliopangwa ni 259 (me- 122 na ke- 137) ambapo kwa
ujumla wapo wanachuo 434 (ME ni 206 na KE 228).
WAPOKEA VIFAA KUTOKA WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Bw.Segesela amesema
wamefanikiwa kupokea vifaa mbalimbali kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na
Teknolojia,ambavyo vilinunuliwa kwa nyakati tofauti.
Amevitaja vifaa hivyo
ni pamoja na gari jipya aina ya landcruiser hard top,Kuletewa vitabu
vya aina mbalimbali zaidi ya nakala 770,kuletewa computer 30 aina ya
desk zilizokamilika na zingine 20 zipo katika hatua ya kumilishwa
mchakato wake,kuletewa mashine ya photocopy machine (heavy duty)
moja,pamoja na projecta tano.
Pia,kununuliwa vifaa
mbalimbali vya kufundishia na kujifunzia wanafunzi wenye ulemavu vyenye
thamani ya zaidi ya milioni 138,kuletewa vitabu mbalimbali vya baadhi ya
masomo ya kidato cha kwanza na cha pili kwa ajili ya shule ya
sekondari,Kuletewa viti mwendo vitatu kwa ajili ya wanafunzi wa
sekondari wenye mahitaji maalum.
“Pamoja na mapokezi
ya vifaa hivyo, pia wafanyakazi wa chuo wamepatiwa mafunzo mbalimbali ya
kuwajengea ujuzi katika maeneo yao ya taaluma na masuala ya mtambuka
kulingana na kada/taaluma zao kwa lengo la kuwajengea uwezo katika
utekelezaji wa majukumu yao,”amesema.
SHULE YA SEKONDARI PATANDI
Kuhusiana na Mpango
wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Patandi,Mkuu huyo amesema
ulilenga kujenga majengo kumi ambayo ni utawala,bwalo,jiko,madarasa
manne na mabweni manne.
“Bloko za Madarasa
zilizojengwa zina jumla ya vyumba 12 na ofisi 6 pamoja na vyumba ambavyo
vinaweza kutumika kwa ajili ya komputa, maktaba, maabara ya sayansi 1.
Pia bloko za mabweni zina vyumba 14 kila moja ambavyo vinaweza kuchukua
wanafunzi 4 hadi 6 kila chumba na ukumbi wa bwalo unakadiriwa kuchukua
wanafunzi 300 hadi 400 ikitegemea mpangilio wa ukaaji katika vyumba
utakavyowekwa,”amesema.
Amesema hadi kufikia Agosti mwaka 2021 ujenzi wa majengo hayo yote kumi umekamilika kwa wastani wa asilimia zaidi ya 99.9%.
WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA YANUNUA THAMANI
Mkuu huyo wa Chuo
amesema Wizara ya Elimu Sayansi na teknolojia imefanikiwa kununua na
kutengeneza samani za shule ambazo ni Vitanda double ‘decker‘ 68 sawa na
single 136,viti vya wanafunzi darasani 185,meza vya wanafunzi darasani
185,meza za bwalo la chakula 65,viti vya bwalo la chakula 400
Pia,utengenezaji wa
viti vya ofisini 18,viti maalum vya ofisi 3,Meza kubwa ya ofisini,Kabati
1 ya usajili ‘Steel waiting chairs (three seaters)’,Meza ya mbao ya
ofisini (std) 3,Kiti (std) cha mbao 1,Magodoro 136.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇