Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT CCM), Philis Nyimbi (Picha ya juu katikati) amewaagiza viongozi wa UWT wilaya na mikoa nchini kufanya mazoezi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi. Agizo hilo amelitoa leo alipozindua rasmi mazoezi kwa wanawake wa Mkoa wa Dodoma yaliyoandaliwa na UWT Mkoa wa Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri. Amesema kuwa kufanya mazoeli ni hazina kwa afya ya mwili lakini vile vile inasaidia kupambana na magonjwa mbalimbali ikiwemo janga la Corona. Ametoa wito kwa wananwake kujitokeza kwenye mazoezi hao ikiwa ni kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ambaye akiwa Makamu wa Rais aliagiza watu kufaya mazoezi kila jumamosi.
Amewapongeza UWT Dodoma kufanya mazoezi kila jumamosi hivyo kumuunga mkono Rais Samia kwa vitendo.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Philis Nyimbi (katikati) kuzungumza na waliohudhuria maozoezi hayo.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Philis Nyimbi (katikati) kuzungumza na waliohudhuria maozoezi hayo.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii, Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Philis Nyimbi, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Neema Majule na Mjumbe wa Baraza la Wanawake Taifa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Songwe, Neema Mwandabila wakizungumza wakati wa mazoezi hayo.....
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇