WAENDESHA Bodaboda na Bajaji mkoani Dodoma ameupongeza Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kuanzisha mafunzo ya kurasimisha biashara zao.
Pongezi hizo zimetolewa na wafanyabiashara hao wakati wa uzinduzi wa Programu ya mafunzo ya urasimishaji wa wafanyabiashara wa Bodaboda na Bajaji uliofanywa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Agosti 27,2021.Naibu Waziri Ndejembi amewataka wafanyabiashara wa vyombo hivyo vya moto kuchangamkia fursa hiyo kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mafunzo hayo na kuwa mabalozi kwa kuwapa taarifa wenzao ili nao wahudhurie.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITA, Mujungu alisema kuwa mafunzo hayo yataanza Jumatatu Agosti 30, 2021 kwa Kata 40 za Dodoma Mjini na baadaye Programu hiyo itaendelea katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.
Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video usikie pongezi kwa MKURABITA kutoka kwa wafanyabiashara hao.....
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇