Shirika la Tanzania Health Summit wameandaa Mdahalo wa Kitaifa kuhusu Chanjo ya COVID19 wiki hii siku ya Alhamisi tarehe 12/8/2021 Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, kuanzia saa 3 asubuhi.
Kufuatia Utambuzi wa Juhudi zake za kutoa Elimu kwa Umma kuhusu namna ya kujikinga Ugonjwa wa COVID19 na Chanjo ya COVID19; Shirika la Tanzania Health Summit wamemualika Mbunge Neema Lugangira kushiriki na Kutoa Mada. Mgeni Rasmi atakuwa Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya.
Hiki ni Kikao Muhimu ili tupate Elimu Sahihi. Kushiriki, tafadhali jisajili kupitia www.mdahalo.ths.or.tz
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇