Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
DARAJA la Mto Nyamwifa ni muhimu sana kwenye barabara inayounganisha Vijiji vya Bukima, Bulinga na Bwasi – yaani barabara hii inaunganisha KATA 3 zenye BIASHARA za mazao ya UVUVI na KILIMO.
MTENDAJI wa KATA ya Bwasi, Ndugu Mashaka Kagere ameeleza kuwa Daraja hilo liliharibika Mwaka 2018 na kupelekea shughuli za kijamii kuzorota sana. Magari ya kusafirisha SAMAKI kutoka Kome Beach yalishindwa kusafirisha bidhaa hiyo. Hata magari ya abiria yalisimama kufanya kazi huko.
MENEJA wa TARURA (W), Injinia Hussein Abbas ameeleza kuwa wamepata SHILINGI MILIONI 300 kutoka MFUKO wa BARABARA (ROAD FUND) kwa ajili ya MRADI wa DARAJA la Mto Nyamwifa na barabara za eneo hilo. FEDHA hizo zitatumika hivi:
*ujenzi wa Daraja
*ulimaji wa barabara ya km 5.0
*ujenzi wa kalavati 3
*uchimbaji wa mitaro na uwekaji wa kifusi sehemu korofi
MKANDARASI M/s Flow Services and Supplies Ltd ndiye anayetekeleza MRADI huu unaopaswa kukamilika kabla ya mvua za vuli kuanza kunyeesha (Oktoba 2021).
WANAVIJIJI wa Kata 3 (Bukima, Bulinga na Bwasi), WAFANYA BIASHARA na VIONGOZI mbalimbali wanaishukuru sana SERIKALI kwa kutoa FEDHA za kutatua TATIZO hili lilowasumbua tokea Mwaka 2018.
MBUNGE wa JIMBO, Profesa Sospeter Muhongo amekuwa akifuatilia kwa ukaribu sana MIRADI ya BARABARA zote za Musoma Vijijini.
MBUNGE huyo anaishukuru sana SERIKALI kwa kupitisha BAJETI ya SHILINGI BILIONI 2.85 kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa barabara za Musoma Vijijini kwa Mwaka huu wa Fedha (2021/2022).
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇