Kaimu Mkurugenzi wa
Takwimu za Uchumi wa NBS, Daniel Masolwa akizungumza na
vyombo vya habari jijini Dodoma leo Agosti 5,2021. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma
OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS), imetoa taarifa ya Ukuaji wa Uchumi kwa robo ya kwanza ya 2021, ambapo shughuli ya uchimbaji wa madini na mawe imeongoza kwa kuwa na kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa asilimia 10.2.
Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa NBS, Daniel Masolwa alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma leo Agosti 5,2021.
Ametaja ametaja kuwa Habari na Mawasiliano ilmefuatiwa kwa kuwa na asilimia 9.1, Ufidhadhi wa Mizigo (asilimia 9.0), Maji Safi na Maji Taka 9.0%, Huduma za Kitaalamu, Sayansi na Ufundi 7.8% Huduma zinazohusiana na Utawala 7.4% na Umeme 7.2%.
Kwa upande wa Mchango wa Shughuli Kuu za Kiuchumi inayoongoza ni Shughuli za Huduma asilimia 40.1 ya pato la Taifa zikifuatiwa na shughuli za maingi 37.1% na shughuli za kati 22.7%.
Ukuaji wa Pato la Taifa katika robo ya kwanza ya mwaka 2021 wa asilimia 4.9 umechangiwa na na shughuli zote za kiuchumi zilizofanyika nchini katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu.
Amesema kuwa mchango mkubwa katika ukuaji wa umetokana na shughuli za kiuchumi za za ujenzi kwa asilimia 14.9, uchukuzi na uhifadhi wa mizigo 14.6 Kilimo kwa asilimia 12.7, Uzalishaji viwandani asilimia 9.8 na uchimbaji wa madini na mawe kwa asilimia 8.8.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇