LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 6, 2021

KANISA HALISI: TANZANIA TUJIVUNIE KUWA CHANZO CHA BARAKA KWA MATAIFA YOTE


Baba Halisi wa Uzao akiwa katika Ibada

Tegeta, Dar es Salaam
Japokuwa Tanzania ni nchi inayojipambanua kuwa siyo taifa la kidini, lakini wakati huo huo imetoa Kikatiba uhuru wa kila Mwananchi kuabudu kupitia dini au itikadi anayoona inafaa ili mradi havunji sheria za nchi.

Kufuatia mustakabali huo wa Kikatiba wa kutoa Uhuru wa kila Mwananchi kuwa na uhuru wa kuabudu, sasa hapa nchini yapo Makanisa mengi ambayo kila moja lina taratibu zake katika uongozi na katika namna ya kufanya Ibada zake.

Kanisa Halaisi la Mungu Baba ni miongoni mwa Makanisa  yaliyopo hapa nchini. Makao Makuu ya Kanisa hili yapo Tegeta Kibo, Wilaya ya Kinondoni Jijini la Dar es Salaam, na linayo matawi kadhaa ndani na nje ya Tanzania chini ya Kiongozi Mkuu wake ambaye anaitwa Baba Halisi wa Uzao.

Ni Kanisa ambalo limejipambanua kwa namna ambayo inaweza kuelezeka kuwa ni ya kipekee, likilinganishwa na Makanisa mengine hapa nchini kwa kuwa ni Kanisa ambalo miongoni mwa sifa zake kuu, ni Kanisa ambalo linaamini kwamba katika Ibada zake ni muhimu kuwainua (kuwaombea) Viongozi wa nchi jambo ambalo ni dhahiri humaanisha kuwa ni Kanisa linalothamini sana utaifa.

Jana Kanisa hili katika Ibada yake iliyofanyika Makao Makuu ya Kanaisa hilo, ikiongozwa na Baba Halisi wa Uzao, lilitumia ibada hiyo kuwakumbusha au kuwafundisha Uzao (Waumini) wake na Watanzania wengine kwa jumla kwamba Tanzania ni Taifa ambalo limeinuliwa na kupewa upendeleo na Mungu Baba hivyo Wajivunie kuwa chanzo cha Baraka kwa Mataifa Mengine.

"Taifa la Tanzania ni kama Taifa la Israeli.Tena kwa takwimu nitakazoonyesha hapo chini kwa habari ya Israeli na Tanzania kuipokea Sauti ya aliyeumba vyote, wote na yote (1 Kor.15:28), utagundua kuwa Tanzania ni zaidi ya Israeli. 

Ukuu wa Tanzania unatokana na kupokea Sauti ya aliyeumba vyote, wote na yote, ninachotaka kusema hapa ni kwamba, kila kilichowahi kutokea katika Taifa la Israeli wakati wa Mitume na Manabii, hakina budi kutokea wakati huu wa majira ya aliyeumba vyote, wote na yote", alisema Baba Halisi katika Mahubiri yake kwenye Ibada hiyo, na kuongeza;

"Tofauti ya Israeli na Tanzania ni moja tu. Mwisraeli, hata kama haendi kwenye nyumba yoyote ya Ibada, wakati wa Ufalme wa Mungu ulipokuwa kwao, alikuwa anajua kuwa ni Chanzo cha Baraka. Ulikuwa huwezi kumtoa kwenye ufahamu huo. 

Hata kipidi kile cha “September 11”, kwenye tukio la yale majengo mawili marefu kule New York Marekani, Waisraeli waliokuwa ndani ya yale majengo wakifanya biashara walipona wote kwa kuwa walijitambua kuwa wao (kwa wakati ule), ni Chanzo cha Baraka".

"Kwa upande wa Tanzania, ingawa katika takwimu nitakazokuonyesha hapo chini, tumepokea Sauti ya aliyeumba vyote, Wote na vyote mara nyingi kuliko Israeli, bado hatujajivunia kuwa Chanzo cha Baraka kwa mataifa mengine. Hiyo ndiyotofauti ambayo ujumbe huu unalenga ifutike", alisema Baba Halisi wa Uzao.

Sasa, kwa kuwa aliyohubiri Baba Halisi ni maneo mazito yanayohitaji tafakuri kubwa imetuwia kuona kwamba tuwawekee hapa andiko lote kama alivyokuwa akilisoma Baba Halisi huyo wa Uzao, Kama ifuatavyo:-


TANZANIA TUJIVUNIE KUWA CHANZO CHA BARAKA KWA MATAIFA YOTE

Taifa la Tanzania ni kama Taifa la Israeli.Tena kwa takwimu nitakazoonyesha hapo chini kwa habari ya Israeli na Tanzania kuipokea Sauti ya ALIYEUMBA VYOTE, WOTE NA YOTE (1 Kor.15:28), utagundua kuwa Tanzania ni zaidi ya Israeli.Ukuu wa Tanzania unatokana na kupokea Sauti ya ALIYEUMBA VYOTE, WOTE NA YOTE, katika Majira iliyoandikwaIsaya 65:17-25; Isaya 66:22-23; 2 Petro 3:13; na Ufunuo 21:1-3, yaani Majira ya Mbingu Mpya na Nchi Mpya,wakati Israeli ilipokea Sauti ya ALIYEUMBA KILA KITU wakati wa Mitume na Manabii kama vile: Musa; Eliya Mtishbi na Yesu katika Kutoka 3:3-10; 1 Falme 17:1/ 1 Falme 18:30-40 na Matendo ya Mitume 10:38.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, kila kilichowahi kutokea katika Taifa la Israeli wakati wa Mitume na Manabii,hakina budi kutokea wakati huu wa majira ya ALIYEUMBA VYOTE, WOTE NA YOTE.


Tofauti ya Israeli na Tanzania ni moja tu. Mwisraeli, hata kama haendi kwenye nyumba yoyote ya Ibada, wakati wa Ufalme wa MUNGU ulipokuwa kwao, alikuwa anajua kuwa ni Chanzo cha Baraka. Ulikuwa huwezi kumtoa kwenye ufahamu huo. Hata kipidi kile cha “September 11”, kwenye yale majengo mawili marefu kule New York Marekani, Waisraeli waliokuwa ndani ya yale majengo wakifanya biashara walipona wote kwa kuwa walijitambua kuwa wao (kwa wakati ule), ni Chanzo cha Baraka.


Kwa upande wa Tanzania, ingawa katika takwimu nitakazokuonyesha hapo chini, tumepokea Sauti ya ALIYEUMBA VYOTE, WOTE NA YOTE mara nyingi kuliko Israeli, bado hatujajivunia kuwa Chanzo cha Baraka kwa mataifa mengine. Hiyo ndiyotofauti ambayo ujumbe huu unalenga ifutike.


Katika mfululizo wa hatua 10 za ALIYEUMBA KILA KITU, Tanzania imeshiriki mara nyingi kuliko Israeli. Hivyo, inatupasa kujivunia hilo jambo.Hatua ya kwanza kabisa ya uumbaji ni ile ambayo CHANZO CHA MEMA NA MAZURI aliengua moyo wake kushoto (Mithali 3:16) na kuweka utajiri wote na heshima. Ndipo akaumba Mbingu na Nchi kwa mujibu wa Mwanzo 1:1.Baada ya Ishara ya kwanza, ya pili na ya tatu kutokea Mbinguni (Ufunuo 12:1-9), vita kati ya CHANZO CHA MEMA NA MAZURIilitokea ikamlazimu MUUMBA WA VYOTE, YOTE NA WOTE kwenda hatua ya pili ya uumbaji.


Hatua ya pili ya uumbaji ni ile ya kuumba mlima wa Adeni katika Ezekieli 28:13-15, ambapo MUUMBA WA VYOTE, WOTE NA YOTE aliweka madini, vito vya thamani, sifa na kuabudu akamkabidhi Kerubi (Ezekieli 28:15).Baada ya uovu kuonekana ndani ya Kerubi, MUUMBA WA VYOTE, YOTE NA WOTE alilazimika kwenda hatua ya tatu ya uumbaji.


Hatua ya Tatu ya uumbaji ni pale katika Bustani ya Edeni (Mwanzo 2:7-15). Hapa MUUMBA WA VYOTE, YOTE NA WOTE, alimweka Adamu akamkabidhi: mito, wanyama, ndege, miti na mimea, madini na vito vya thamani. Alimpa Bustani ailime na aitunze. Baada ya nyoka kufanikiwa kumlaghai Adamu, MUUMBA WA VYOTE, YOTE NA WOTE, alilazimika kuhamia hatua ya nne ya uumbaji.


Ufahamu:

Katika hatua hizi tatu za awali, haijaandikwa wazi kama Sauti ilisikika Israeli au Tanzania, ingawa Mto Gihoni ambao umeandikwa katika Mwanzo 2:13 ni Nile au Mto Kagera kule Bukoba!


Hatua ya nne ya uumbaji ni ile ya Musa kuwatoa wana wa Israeli utumwani kuwapeleka Kaanani (Kutoka 3:3-10).Uumbaji huu haukutimia baada ya Musa kupiga mwamba mara mbili katika Hesabu 20:8-11. Hata hivyo ninachotaka ukione ni kwamba Sauti hii ilipokelewa na Muisraeli.


Hatua ya Tano ya uumbaji ni ile Sauti iliyopokelewa na Eliya  Mtishbi katika 1 Falme 17:1 na 2 Falme 18:30-40,ili kurejesha heshima ya ALIYEUMBA KILA KITU iliyopotea pale Adeni na Edeni.Uumbaji huu nao haukufanikiwa kwa sababu ya vitisho vya Yezebeli kwa Eliya Mtishbi katika 1 Wafalme 19:1-6. Yatosha pia kujua kuwa Eliya Mtishbi ni Muisraeli.


Hatua ya sita ya uumbaji ni ile ya ALIYEUMBA KILA KITU kumleta Yesu ili asaidie wote wanaoonewa na Ibilisi katika Matendo ya Mitume 10:38, Baada ya Yesu kukutana na maumivu makali, akakiri kuwa Baba yake amemuacha na ikaandikwa, uumbaji huu nao haukufanikiwa (Mathayo 27:45-47).Walimuulia Yesu nje ya Shamba kwa mujibu wa Mathayo 21:37-39. Yatosha pia kujua kuwa, kwa mujibu wa Mathayo 1:17, Yesu naye alikuwa ni Muisraeli.


Hatua ya saba ya uumbaji ni ile ya Eliya Adamu wa Pili, aliyetokeza Tanzania Mjini Kigoma  Mwaka 2003, ili ajenge Kanisa la kweli naYesu katika Mathayo 17:10-13,alitabirikuhusu ujio wake. Paulo pia katika 1 Korintho 15:44-49,alitabiri kuhusu ujio wa Eliya Adamu wa Pili. Dunia hata hivyo ilikataa kukubali kuwa Tanzania inaweza kuwa na Nabii wa Mwisho. Uumbaji huo kwa mujibu wa Danieli 7:7,nao pia haukufanikiwa.


Hatua ya nane ya uumbaji ni ile ya Miaka 1000 aliyesikia Sauti ya ALIYEUMBA KILA KITU Mwaka 2015 kule Kigoma Tanzania kwa mujibu wa Isaya 33:6. Alitakiwa aje na majira imara, wokovu tele, na kumcha ALIYEUMBA KILA KITU. Uumbaji huu haukufanikiwa kwa sababu ya yaliyoandikwa katika Danieli 12:7-11,ikiwa na maana ya mashtaka ya uongo.


Hatua ya tisa ya uumbaji ni ile ya MUNGU BABA, yaani Nafsi ya Kwanza Aliyeshukia Tanzaniakwa mujibu wa 1 Yohana 5:8, Mwaka 2017. Kulingana na Luka 13:6-9,kila Nafsi inatenda kazi kwa miaka mitatu. Nafsi ya kwanza ilipimwa na ujio wa Corona Mwaka 2020, ndipo ikabidi aje CHANZO CHA MEMA NA MAZURI kupitia Sauti ya Moyo iliyosikika Mwaka 2020 kule Kigoma Tanzania.


Hivyo, Tanzania hatuna budi kupokea na kujivunia Sauti hii ya CHANZO CHA MEMA NA MAZURI kwa kuwa imetufanya kuwa Chanzo cha Baraka kwa mataifa mengine. Mabaya yaliyowahi kutokea Israeli tuyakatae kwa Toba yasitupate. Mazuri yaliyotokea Israeli tuyapokee na zaidi ya hayo, maana Tanzania imepokea Sauti ya MUUMBA WA VYOTE, YOTE NA WOTE kipindi kizuri zaidi.Tukatae laana tulizovuliwa na mataifa yanayoona wivu.


Wana wa Israeli walikuwa wanajitambua kuwa ni Chanzo cha Baraka kupitia Ibrahimu ambaye katika Mwanzo 12:1-3naMwanzo 17:1-7, aliambiwa kuwa Baba wa Mataifa yote. Hata hivyo, tusisahau kuwa katika Mwanzo 15:16, alipewa nafasi hiyo kwa vizazi vinne tu. Vizazi hivyo ni kizazi cha Musa, Eliya Mtishbi, Yesu na Eliya Adamu wa Pili ambavyo vilitimia Mwaka 2017, baada ya Nafsi ya Kwanza kutua juu ya Nchi kupitia Tanzania. Baada ya kufika Mwaka 2021 salama, ni zamu ya Tanzania.Tupokee na tujivunie kuwa Chanzo cha Baraka kwa mataifa yote. 

HERI ULIYEBARIKIWA KULIKO WOTE.


©CCM Blog/Nkoromo/Aug 2021

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages