LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 1, 2021

RAIS SAMIA KWENDA NCHINI RWANDA KESHO KUANZA ZIARA YA SIKU MBILI

 Ikulu, Dar es Salaam, leo

Rais Samia Suluhu Hassan, kesho Jumatatu Agosti 2, 2021 anatarajia kuondoka hapa nchini kwenda nchini Rwanda kufanya ziara ya Rasmi ya Kiserikali ya siku mbili nchini humo kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Paul Kagame.


Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Raais, Ikulu Jijini Dar es Salaam Jaffar Haniu, imesema akiwa nchini Rwanda Rais Samia pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Kagame, kisha atashuhudia utiaji saini wa hati za makubaliano na kuzungumza na vyombo vya habari.


Taarifa hiyo imefafanua kuwa ziara hiyo ya siku mbili inalenga kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano baina ya Rwanda na Tanzania.

Rais Samia Suluhu Hassan

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages