LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 16, 2021

RAIS SAMIA AWASILI JIJINI LILOGWE NCHINI MALAWI JIONI HII, TAYARI KWA MKUTANO WA SADC UNAOANZA KESHO

 


Lilongwe, Malawi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewasili Jijini Lilongwe nchini Malawi kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika kesho na keshokutwa (17 – 18 Agosti,2021).


Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jaffar Haniu amesema, baada ya Rais Samia kuwasili jioni hii katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu, amepokelewa na Waziri wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii wa Malawi Patricia Kaliati.


Amesema katika Mkutano huo wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC, Jamhuri ya Malawi itathibitishwa kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha mwaka mmoja (Agosti 2021 – Agosti 2022)  na pia Wakuu hao wa Nchi na Serikali watamthibitisha Katibu Mtendaji mpya wa SADC baada ya Katibu Mtendaji aliyepo Dk. Stergomena Tax wa Tanzania kumaliza muda wake baada ya kuhudumu kwa ufanisi nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka nane.


Haniu amesema katika taarifa yake kuwa vyombo vya habari kuwa, Wakuu hao wa Nchi na Serikali wa SADC pia wanatarajiwa kujadili masuala mbalimbali ya Mtangamano pamoja na kuidhinisha kauli mbiu  ya Jumuiya hiyo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii wa Malawi Patricia Kaliati baada ya kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu jijini Lilongwe, baada ya kuwasili nchini humo jioni hii kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 41wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kuanza kesho (Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages