Naibu
Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato akiwasha umeme katika Shule
ya Msingi Mongahay iliyopo Kata ya Tumati wilayani Mbulu, Mkoa wa
Manyara kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini
Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika Mkoa huo. Tukio hilo lilifanyika
Agosti 14, 2021. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Sezaria Makota
(katikati), Mbunge wa Mbulu Vijijini, Fratei Massay (mwenye kofia) na
Mbunge wa Mbulu Mji, Zacharia Issaay (kulia).
Mkurugenzi
Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga
akizungumza wakati wa Hafla ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kusambaza
Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili kwa Mkoa wa Manyara. Mgeni
Rasmi katika tukio hilo lililofanyika katika kijiji cha Mongahay, Kata
ya Tumati, Wilaya ya Mbulu, Agosti 14, 2021 alikuwa Naibu Waziri wa
Nishati, Wakili Stephen Byabato (hayupo pichani).
Mbunge
wa Mbulu Mji, Zacharia Issaay akizungumza wakati wa Hafla ya uzinduzi
rasmi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa
Pili kwa Mkoa wa Manyara. Mgeni Rasmi katika tukio hilo lililofanyika
katika kijiji cha Mongahay, Kata ya Tumati, Wilaya ya Mbulu, Agosti 14,
2021 alikuwa Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (hayupo
pichani).
bunge
wa Mbulu Vijijini, Fratei Massay akizungumza wakati wa Hafla ya
uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu
Mzunguko wa Pili kwa Mkoa wa Manyara. Mgeni Rasmi katika tukio hilo
lililofanyika katika kijiji cha Mongahay, Kata ya Tumati, Wilaya ya
Mbulu, Agosti 14, 2021 alikuwa Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen
Byabato (hayupo pichani).
Mkuu
wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria Makota akizungumza wakati wa Hafla ya
uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu
Mzunguko wa Pili kwa Mkoa wa Manyara. Mgeni Rasmi katika tukio hilo
lililofanyika katika kijiji cha Mongahay, Kata ya Tumati, Wilaya ya
Mbulu, Agosti 14, 2021 alikuwa Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen
Byabato (hayupo pichani).
Naibu
Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Mongahay, Kata ya Tumati wilayani Mbulu, Mkoa wa Manyara,
wakati wa Hafla ya Uzinduzi rasmi wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini
Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika Mkoa huo.
Kutoka
kushoto ni Katibu wa Naibu Waziri wa Nishati Mhandisi Ngereja Mgejwa,
Msimamizi wa Miradi ya Umeme Vijijini Kanda ya Kaskazini kutoka Wizara
ya Nishati Mhandisi Shukurani Rugaimukamu na Kaimu Meneja Usimamizi na
Uendelezaji Miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi
Emanuel Yessaya wakiwa katika Hafla ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa
Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili kwa Mkoa wa
Manyara. Mgeni Rasmi katika tukio hilo lililofanyika katika kijiji cha
Mongahay, Kata ya Tumati, Wilaya ya Mbulu, Agosti 14, 2021 alikuwa Naibu
Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (hayupo pichani).
Msimamizi
wa miradi ya usambazaji umeme vijijini, Kanda ya Kaskazini, Mhandisi
Gilbert Furia (wa tatu-kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wenzake kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Julian Kiiza
(kulia) na Kassongo Rubeya (kushoto, mara baada ya Naibu Waziri wa
Nishati, Wakili Stephen Byabato (hayupo pichani) kuzindua rasmi Mradi wa
Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili kwa Mkoa wa
Manyara. Tukio hilo lilifanyika katika kijiji cha Mongahay, Kata ya
Tumati, Wilaya ya Mbulu, Agosti 14, 2021. Wengine pichani ni wafanyakazi
kutoka TANESCO.?
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Mongahay iliyopo Kata ya Tumati wilayani Mbulu, Mkoa
wa Manyara wakitumbuiza kwa kucheza ngoma wakati wa Hafla ya uzinduzi
rasmi wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa
Pili katika Mkoa huo. Mgeni Rasmi katika tukio hilo lililofanyika Agosti
14, 2021 alikuwa Naibu Waziri wa Nishati Wakili Stephen Byabato.
…………………………………………………………………………………..
Veronica Simba na Zuena Msuya – Manyara
Viongozi
mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato,
Wabunge wa Majimbo yaliyopo Wilaya ya Mbulu na Mkuu wa Wilaya hiyo,
Sezaria Makota, wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Samia Suluhu kwa utekelezaji makini wa miradi ya umeme vijijini.
Walitoa
pongezi hizo kwa nyakati tofauti wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi
wa Kusambaza Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Pili katika Mkoa
wa Manyara, iliyofanyika Agosti 14 mwaka huu, kijiji cha Mongahay, Kata
ya Tumati, wilayani Mbulu.
Akizungumza
na wananchi kabla ya kuzindua rasmi Mradi huo, Naibu Waziri Byabato
alisema kuwa Rais Samia, kupitia Serikali ya Awamu ya Sita anayoiongoza,
amewezesha upatikanaji wa fedha za kutosha kwa ajili ya kuhakikisha
vijiji vyote ambavyo havijafikishiwa umeme vinapelekewa nishati hiyo
kabla ya Desemba 2022.
Byabato
alitumia jukwaa hilo kutoa rai kwa wananchi kuchangamkia fursa ya
kufikiwa na miundombinu ya umeme katika maeneo yao kwa kuhakikisha
wanalipia shilingi 27,000 tu ili waunganishiwe na kuutumia katika
shughuli mbalimbali za maendeleo ili kuboresha maisha yao.
“Mheshimiwa
Rais ametuwezesha tukawaletea umeme, niwaombe Waheshimiwa Wabunge
mhamasishe wananchi wenu wakimbilie fursa hii ili iwaletee maendeleo.”
Akifafanua,
Naibu Waziri alieleza kuwa katika baadhi ya maeneo ambayo yaefikishiwa
miundombinu ya umeme, mwitikio wa wananchi kulipia ili kuunganishiwa
nishati hiyo, umekuwa mdogo, jambo alilolielezea kuwa ni kurudisha nyuma
jitihada za Serikali za kuwaletea wananchi maendeleo.
“Serikali
inatumia gharama kubwa kuhakikisha miundombinu ya umeme inatufikia.
Sasa, miundombinu ikifika kwenye maeneo yetu, tuhakikishe sisi sote
tunahamasishana kuchangamkia fursa hiyo,” alisisitiza Naibu Waziri
Byabato.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria Makota alipongeza kazi
kubwa inayoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika
kusambaza umeme vijijini huku akitilia mkazo kuwa vijiji vyote vya
Wilaya hiyo, ambavyo havijafikiwa na umeme, vimeingia katika kufikishiwa
nishati hiyo kupitia Mradi huo uliozinduliwa siku hiyo.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mji, Zacharia Issaay alieleza kuwa kazi ya
kusambaza umeme vijijini iliyofanywa na Serikali kupitia Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) ni ya kupongezwa sana kwani imesaidia kwa kiasi
kikubwa kuboresha maisha ya wananchi.
“Nichukue
nafasi hii kuipongeza sana Serikali ya Awamu ya Tano na ya Sita kwa
kazi kubwa ya usambazaji umeme vijijini kupitia REA.”
Mbunge
Issaay alibainisha kuwa kadri umeme unavyounganishwa katika maeneo
mbalimbali ndivyo wananchi wengi wanavyohamasika kufungua miradi ya
kimaendeleo zikiwemo mashine za kusaga nafaka, hivyo akaiomba Serikali
kuongeza wigo wa upelekaji huduma hiyo kwa manufaa ya jamii husika.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Fratei Massay
alimwomba Naibu Waziri Byabato kufikisha salamu za wananchi wa eneo hilo
alizoziita ‘za kindakindaki’ kwa Rais Samia kutokana na kazi kubwa
anayoifanya ya kuwapelekea maendeleo ikiwemo umeme.
“Naishukuru
Serikali kwenye Bajeti hii iliyopita, tumepata vijiji karibu vyote
kasoro kimoja tu. Ukikosa kimoja haulalamiki bali unashukuru,”
alisisitiza Masai.
Awali,
Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga alibainisha kuwa Mkoa wa
Manyara una jumla ya vijiji 441 ambapo vijiji 278 tayari vina umeme na
vilivyosalia 163 vinapelekewa nishati hiyo kupitia Mradi wa Umeme
Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili.
Kwa
upande wa Wilaya ya Mbulu, Mhandisi Maganga alieleza kuwa kuna jumla ya
vijiji 110 ambapo vyenye umeme ni 48. Alifafanua kuwa vijiji
vitakavyopelekewa umeme kupitia Mradi huo wa Awamu ya Pili ni 62 na kwa
gharama ya shilingi bilioni 18.8.
Mradi
wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili kwa Mkoa wa
Manyara unatekelezwa na Kampuni ya Ukandarasi ya Nakuroi Investment
pamoja na Giza Cable Industries Ltd kwa gharama ya shilingi bilioni
65.3.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇