MBUNGE wa wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo ana mpango wa kugawa bure majembe ya kukokotwa na Ng'ombe (PLAU) kwenye vikundi vya kilimo katika vijiji vyote 68 vya Jimbo hilo.
Katika taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Msaidizi wa Mbunge huyo, Verediana Mgoma amesema kuwa Profesa Muhongo ameamua kutoa msaada ili kuboresha kilimo jimboni kwake.
Aidha amesema kuwa kwa kushirikiana na serikali, Mbunge huyo, ameshagawa bure tani 9.85 za mbegu za Alizeti ambapo Wizara ya Kilimo imechangia tani 10 za mbegu hiyo.
Pia Mbunge huyo katika lengo lake la kuwataka wananchi kuachana na jembe la mkono na kuboresha kilimo, tayari amegawa bure mbegu za mihogo, mtama na ufuta, ambapo kwa Kata moja tu ya Bukumi ameshagawa mbegu hizo kwenye Vijiji vyote 4 na Plau 5 kwenye vikundi vya kilimo ambavyo ni: Amani Group, Mshikamano, Umoja ni Nguvu, Nyabigoma na Majita Group.
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda,
Mhariri Blog ya Taifa CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇