Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
SALAMU ZA HERI ZA NANENANE KWA WAKULIMA WA MUSOMA VIJIJINI
SHEREHE za NANENANE hazikufanyika Mwaka huu kuepuka
MADHARA ya KORONA. Tarehe nyingine itapangwa kwa ajili ya Mashindano
yetu ya kila Mwaka ya NaneNane – Ngoma za Asili & Kwaya.
JUMATATU, tarehe 9.8.2021 umefanyika uzinduzi wa CHANJO
ya COVID-19 kwenye Viwanja vya S/M KWIBARA, karibu na Makao Makuu ya
Muda ya Halmashauri yetu.
MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameishachanjwa (J&J jab) na Wasaidizi wake wote 5 watachanjwa.
CHANJO HII NI SALAMA, SISI SOTE TWENDE TUKACHANJWE
UBORESHAJI WA KILIMO JIMBONI MWETU
JIMBO la Musoma Vijijini linafanya yafuatayo kuboresha
KILIMO cha WAKULIMA wake:
*WAKULIMA wanashawishiwa waunde VIKUNDI vya KILIMO ili kurahisisha upatikanaji ya MAHITAJI yao ya Kilimo
*KILIMO cha UMWAGILIAJI kinawekewa mkazo sana, kwani hatuko mbali na Ziwa Viktoria.
*ZAO JIPYA la ALIZETI linastawi vizuri kwenye udongo wetu.
*PLAU, Jembe la kukokotwa na ng’ombe linagawiwa bure
kwenye Vikundi vya Kilimo. Hizi ni jitihada za kupunguza utumiaji wa
JEMBE la MKONO.
KIKUNDI CHA ANGAZA CHA KIJIJI CHA BURAGA
KIJIJI cha BURAGA ni kimoja kati ya Vijiji 4 vya KATA ya BUKUMI. Vijiji vingine ni Buira, Bukumi na Busekera.
KIKUNDI cha ANGAZA chenye Makazi yake Kijijini Buraga,
kilianzishwa Mwaka 2015 na kinafanya shughuli zake za KILIMO kwenye
Kijiji cha BUKUMI.
MWENYEKITI wa Kikundi hiki, Ndugu Pius Bwire ameeleza kwamba KIKUNDI chao:
*kina Wanachama 11
*wanajishughulisha na kilimo cha BUSTANI za matikiti, matango, nyanya na maboga aina ya batanati
*baada ya kupata nyenzo bora za kilimo, watapanua
mashamba yao ili kupanua KILIMO cha MAZAO ya BIASHARA yakiwemo ya
alizeti, mahindi na mihogo.
AFISA KILIMO wa Kata ya Bukumi, Ndugu Alex Mihambo
amekuwa akitembelea KIKUNDI hicho na vingine kwa ajili ya kutoa mafunzo,
ushauri na maelekezo ya kitaalamu.
AFISA huyo wa Kilimo amesema MAFANIKIO ya KIKUNDI cha
ANGAZA yamehamasisha na kutoa mvuto mkubwa kwa WAKULIMA wa KATA hiyo
kujiunga kwenye VIKUNDI vya KILIMO na kuanza KILIMO cha BUSTANI chenye
kutumia MAJI ya Ziwa Viktoria kwa UMWAGILIAJI.
Wakulima wameanza kuongeza mavuno ya mahindi kutoka magunia 4-5 kwa ekari hadi 8-10 kwa ekari.
MCHANGO WA MBUNGE WA JIMBO KWENYE UBORESHAJI WA KILIMO VIJIJINI MWAO
MBUNGE wa Jimbo akishirikiana na SERIKALI anafanya/amefanya yafuatayo:
*kugawa bure MBEGU za ALIZETI. Mbunge aligawa bure TANI
9.85 za mbegu za Alizeti, na WIZARA ya KILIMO ilichangia TANI 10 za
mbegu hiyo.
*MBUNGE aligawa bure mbegu za mihogo, mtama na ufuta
*MBUNGE anayo Programu yake ya kugawa bure PLAU kwenye Vikundi vya Kilimo vya Vijiji vyote 68 vya Jimbo hili.
MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO KWENYE KATA YA BUKUMI
*kugawa MBEGU za alizeti, mihogo na mtama kwenye Vijiji vyote 4 vya Kata hii
*kugawa PLAU 5 kwenye Vikundi vya Kilimo vya Kata ya
Bukumi ambavyo ni: Amani Group, Mshikamano, Umoja ni Nguvu, Nyabigoma na
Majita Group
*kutoa MASHINE ya UMWAGILIAJI kwa Kikundi cha Angaza kutoka kwenye FEDHA za MFUKO wa JIMBO
KARIBUNI TUBORESHE KILIMO VIJIJINI MWETU – Tununulie
ndugu zetu PLAU waachane na Jembe la Mkono. VIKUNDI vingi vinaomba
MASHINE za UMWAGILIAJI
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇