****************************
NJOMBE
Wakati serikali ikiwa katika hatua za mwisho za kupandisha hadhi Halmashauri ya mji wa Njombe kuwa Manispaa ,madiwani wa Halmashauri hiyo wamesema licha ya kubariki mchakato huo kufanyika lakini halmashauri hiyo bado ina changamoto kubwa za barabara zinazounganisha mitaa,maji na ujenzi horera ,vigezo ambavyo vinazingatiwa katika kupandisha hadhi halmashauri kuwa manispaa.
Katika kikao Cha Baraza ambacho moja Kati ya agenda zake ni kubariki kwa kauli moja mchakato wa kupandishwa hadhi kwa Halmashauri ya mji wa Njombe ,madiwani akiwemo Edwin Mwanzinga ambaye ni mwenyekiti mustaafu na Urick Msemwa wamesema halmashauri imekuwa ikifanya vizuri tangu ianzishwe katika makusanyo ya mapato ambapo kwa mwaka huu imeongoza kitaifa lakini imekuwa na shida kubwa ya huduma ya maji,ujenzi wa vibanda vya mbao pamoja na uchache wa barabara za lami zinazounganisha mitaa jambo ambalo linapaswa kuboreshwa kipindi hiki cha mchakato.
Wakitoa ushauri katika kikao cha kuridhia kuanza mchakato huo madiwani wamesema halmashauri yao ilipaswa kuwa manispaa muda mrefu lakini changamoto ya kuingiza siasa katika utendaji ndiyo imesababisha kuwepo kwa ujenzi horera na wa vibanda katikati ya mji na kwamba wakati umefika wa kuanza kukimbizana na ujenzi wa nyumba za ghorofa na kuboresha huduma za kijamii kama maji ,afya na elimu.
Akieleza mipango wa halamshauri kaimu katika jitihada za kukidhi vigezo vya kuwa manispaa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Thadeo Luoga amesema ni kuongeza makusanyo ambapo kwa mwaka huu halmashauri hiyo imeongoza kitaifa kwa kukusanya zaidi ya asilimia 110 hatua ambayo itawajengea uwezo wa kuboresha miundombinu katika sekta mbalimbali ikiwemo barabara za lami.
Nae mbunge wa jimbo la Njombe mjini Deo Mwanyika ameweka bayana jitihada ambazo amekuwa akiweka bungeni ili kuiomba serikali itazame ulazima wa kuipa manispaa Njombe mji.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇