Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Dodoma, Neema Majule akichangia hoja wakati wa Mkutano wa Wadau wa kutoa elimu na Uhamasishaji kuhusu Sensa ya Watu na Makazi jijini Dodoma Agosti 18,2021 ambapo alisema kuwa wanawake ni wadau wakubwa wa sensa, hivyo watakuwa mstari wa mbele kuhamasisha ili wananchi wajitokeze kwa wingi katika jambo hilo muhimu kitaifa. Sensa itafanyika Agosti 2022.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Majule (kulia) akiwa na Katibu wa UWT wa mkoa huo, Mariam Kireti wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano huo ulioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka.
Mkutano huo wa wadau ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa ya Mkoa huo, Anthony Mtaka ulihudhuriwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Wengine ni Kamishna wa Sensa, Spika mstaafu, Anne Makinda, Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt Albina Chuwa, wabunge wa mkoa huo, wakuu wa wilaya, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa mabaraza ya wazee na taasisi mbalimbali wakiwemo watu wenye ulemavu.
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇