LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 20, 2021

CCM IKO IMARA KUHAKIKISHA SENSA INAFANIKIWA-MNEC MGONGO+video

  • Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Happiness Mgongo akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka kuandaa mkutano huo ulioshirikisha  makundi mbalimbali katika jamii. Happiness ameahidi CCM kuwa iko imara na itashiriki vilivyo kuhakikisha Sensa inafanikiwa kwa kiasi kikubwa.

  • Ametoa mchango wake huo wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili jinsi ya kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuhusu Sensa ya Watu na Makazi jijini Dodoma Agosti 18,2021.
Sehemu ya wadau wakisikiliza kwa makini wakati Mnecp Taifa, Happiness akichangia hoja.





 Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Neema Majule (kulia) akiwa na Katibu wa UWT Mkoa wa Dodoma, Mariam Kireti  katika mkutano huo.


Mkutano huo wa wadau ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa ya Mkoa huo, Anthony Mtaka ulihudhuriwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai.


Wengine ni Kamishna wa Sensa, Spika mstaafu, Anne Makinda, wabunge wa mkoa huo, wakuu wa wilaya, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa mabaraza ya wazee na taasisi mbalimbali wakiwemo watu wenye ulemavu.


Sensa hiyo itafanyika Agosti 2022 na kuzinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan.


Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia kwenye clip hii ya video Mnec- Taifa, Happiness Mgongo akichangia hoja kwenye mkutano huo....

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
 Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages