Askari wakimtoa hadi nje ya eneo la Bunge, Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa baada ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kusoma maazimio ya kumtia hatiani kwa kosa la kusema kauli ya uongo kwamba wabunge hawakatwi kodi kwenze mishahara yao. Amefungiwa kutohudhuria mikutano miwili ya Bunge na kufutwa uwakilishi katika Bunge la Afrika.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka akitangaza maazimio ya Kamati hiyo na kumhukumu Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa kwa kosa hilo.
Spika wa Bunge, Job Ndugai akiwaamuru askari kumtoa nje ya Bunge Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa baada ya Kamati ya Bunge za Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kumtia hatiani kwa kosa la kusema kauli ya uongo kwamba mishahara ya Bunge haikatwi kodi.
Askari wakimuongoza Silaa kumtoa nje ya eneo la Bunge.
Silaa akipiga simu baada ya kutolewa nje.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇