Wanafunzi wa Shule ya Martine Luther ya jijini Dodoma, wakiimba wimbo wakati wa mahafali ya 14 ya Darasa la 7 yaliyofanyika Agosti 7,2021 shuleni hapo. Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Nishati na Msemaji wa Wizara, Dorina Makaya. Jumla ya wanafunzi 244.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Nishati na Msemaji wa Wizara, Dorina Makaya.akihutubia kwa kuwaasa wanafunzi wasiiache elimu iende zake, waizingatie elimu katika maisha yao maana ndiyo ufunguo wa maisha.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Gilbert Mhuguti akielezea mafanikio ya shule hiyo kiwilaya, kimkoa na kitaifa.Baadhi ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba katika shule hiyo wakikata keki maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya mahafali hayo.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Dorina Makaya akilishwa keki na mtoto wake David Kaali ambaye ni miongoni mwa wanafunzi wa darasa la 7 waliokuwa wanaagwa siku hiyo. David ni Kaka Mkuu wa shule hiyo.Kushoto ni mmewe, Daud Kaali.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Dorina Makaya akimkabidhi mwanaye David Kaali cheti ikiwani tuzo ya uongozi bora shuleni hapo. David ni Kaka Mkuu wa shule hiyo.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Dorina Makaya akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi wanaohitimu shuleni hapo.
Mmoja wa wanafunzi waliokuwa wakiagwa akionesha cheti baada ya kukabidhiwa na Mgeni rasmi Dorina Makaya (kushoto).
Mwanafunzi Gabriel akifurahia kupata cheti pamoja na familia yake. |
Makaya akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi wanaohitimu Darasa la Saba. Wanafunzi hao watafanya mtihani wa kitaifa wa kuhitimu Septemba 8 na 9 mwaka huu. |
Wanafunzi wakiimba wimbo wa kizalendo wa kulipenda Taifa letu wakati wa mahafali yao.
Baadhi ya wazazi na wageni waalikwa
Wanafunzi wanaomaliza darasa la 7 wakitumbuiza kwa wimbo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakiwa katika mahafali hayo.
Mkurugenzi wa shule hiyo, Rabbiely Mmanga akiwapongeza walimu.
Mkurugenzi wa Kituo cha Shule ya Martin Luther,Rabbiel Mmanga akizungumza na wazazi na wanafunzi wanaohitimu darasa la saba kuhusu malei ya watoto hao na kuwaasa kuwalea katika msingi wa kumjua na kumtii Mungu wakati wa mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika Agosti 7,2021.
Meneja wa Kituo cha Shule ya Martin Luther, Wendo Mmanga (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Tumsifu Mwasamale wakifuatilia nasaha zilizokuwa zinatolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha Shule hiyo, Rabbiel Mmanga wakati wa mahafali hayo.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇