Wajumbe wa Kamati wakitembelea ujenzi wa nyumba hizo uliofikia asilimia 60.
Wajumbe wakikagua ujenzi wa jengo la maduka.
Wakikagua baadhi ya vyumba vya majengo hayo.
Eneo la jiko ndani ya moja ya nyumba hizo za ghorofa
Nyumba za kawaida 303 ambazo ni maalumu kwa kuuzwa zikiwa katika hatua ya mwisho ya ukamilishwaji eneo la Iyumbu karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma wakiangalia uimara wa matofali yanayofyatuliwa eneo la mradi wa nyumba za NHC Iyumbu Dodoma. Matofali 20000 hufyatuliwa kila siku kwa kutumia mitambo kumi iliyopo eneo hilo la mradi.
Moja ya mitambo ya kufyatulia tofali.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Maulid Banyani akijibu maswali ya wajumbe kuhusu miradi hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Dkt Sophia Kongela akifafanua jambo kwa wajumbe kuhusu miradi hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Atupele Mwakibete akitoa ushauri na maagizo ya kamati kwa NHC.
Wajumbe wa Kamati wakiwa na na baadhi ya viongozi wa NHC.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), imeupongeza uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kwa utekelezaji mzuri wa ujenzi wa miradi ya nyumba 404 Chamwino na Iyumbu mkoani Dodoma.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Atupele Mwakibete baada ya wajumbe wa kamati hiyo kukagua ujenzi wa miradi hiyo inayogharimu sh. bilioni 21 ambapo Chamwino zinajengwa ghorofa nyumba 101 na Iyumbu nyumbaza kawaida 303. NHC ina mpango wa kujenga jumla ya nyumba 1000 mkoani Dodoma. "Niwapongeze sana watendaji na uongozi wote wa shirika, nikianza na Mwenyekiti wa bodi na bodi yake yote, Mtendaji Mkuu na wafanyakazi kwa kazi ambayo mmeifanya vizuri, tunasema kuona ni kuamini na kamati imeyaona yale ambayo tulikuwa tunawahoji pale bungeni,".amesema Mwakibete. Aidha, akizungumzia changamoto zinazoikabili NHC ikiwemo deni sugu la sh. bilioni 26 wanalowadai wapangaji wao, Mwenyekiti wa Kamati Mwakibete ameitaka NHC kuunda kikosi kazi cha kukusanya madeni yote kwa wadaiwa wote wa shirika hilo ili fedha zitakazokusanywa ziende kujenga miradi mingine katika maeneo mengine nchini. Naye Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Kondoa Vijijini, Dkt. Ashatu Kijaji ameupongeza uongozi wa shirika hilo na kwamba baada ya kutembelea miradi hiyo ya ujenzi wa nyumba 101, Chamwino 303 Iyumbu yenye thamani ya sh. bil 21 wamejiridhisha ujenzi unaendelea vizuri. Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Morogoro, Nora Waziri amesema kuwa baada ya wajumbe kutembelea miradi hiyo na kuona maendeleo ya ujenzi ulipofikia, wamefurahishwa na kwamba endapo NHC itaendelea kuongeza nyumba zingine kama hizo walizoziona, basi wataendana na kasi ya Rais Samia Suluhu Hassan. Aidha, Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amelifagilia shirika hilo kwa kusema kuwa baada ya kutembelea miradi wameona sasa limeendelea kupiga hatua kwa kasi ya kuimarika na kwamba wamefarijika kuona miradi inayoendelea ambayo kwa kiasi kikubwa itasaidia kukwamua tatizo la makazi katika Jiji la Dodoma. Amelishauri shirika hilo kuwekeza miundombinu ya kisasa kwa kutumia teknolojia na kwamba imani yao kama kamati litakuwa shirika kiongozi kwa upande wa makazi lakini pia kujiongezea mapato. Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Maulid Banyani, amesema kuwa uongozi wake umepokea kwa furaha pongezi kutoka kwa kamati hiyo na kwamba ushauri na maagizo waliopatiwa watayafanyia kazi. Akijibu kuhusu namna ya kuwabana wadaiwa wao sugu , Banyani amesema kuwa wametenga sh. mil. 500 kuanzisha mfumo mzuri wa kuweka kufuli janja (Smart Locks) kwenye milango ya nyumba zao ambapo milango itakuwa inajifunga muda wa kulipa kodi ukiisha.Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mwakibete akitoa pongezi hizo kwa uongozi wa NHC.......
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇