Karim Madenge
Ilala, Dar es Salaam
Diwani wa Kata ya Buyuni Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam, kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Karimu Madenge amefariki dunia .
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Ilala, Said Sidde Diwani Madenge amefariki dunia jana asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana alikokuwa akipatiwa matibabu.
Sidde amesema taratibu za inafanyika nyumbani kwa marehemu Buyuni, Ilala na mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa kijijini Kibuta Kisarawe Mkoa wa Pwani leo Agosti 5, saa sita mchana.
Sidde amewaomba wana CCM wote kushiriki katika msiba huo wa mwezao huku akiwaomba kuchukua tahadhari za kujikinga na Corona ikiwemo kuvaa Barakoa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇